Antonio Conte atuhumiwa na FA

FA imemtuhumu Antonio Conte kwa kumfokea mwamuzi wa mchezo wao dhidi ya Swansea

Chama cha soka nchini England FA kimemtuhumu meneja wa Chelsea Antonio Conte kwa utovu wa nidhamu ikiwa ni hatua inayofuatia kuondolewa kwake katika Touch Line na mwamuzi wa mchezo wa Jumatano baina yao na Swansea.

Bosi huyo wa Chelsea alielekezwa kwenda kuketi jukwaani baada ya kuonekana kulalamikia waamuzi wa mchezo huo Neil Swarbrick na mwamuzi wa akiba Lee Mason kwa maamuzi ya mpira kuwa ni ‘goal kick’ badala ya kuwa mpira wa kona lakini pia kwa kile alichokiona kuwa wachezaji wa Swansea walikuwa wakipoteza muda.

Hata hivyo Conte hatakumbana na adhabu ya kusimamishwa kwa michezo ujao dhidi ya Newcastle United hadi pale adhabu yake itakapotangzwa baadaye.

Antonio Conte akiamrishwa na mwamuzi Neil Swarbrick kwenda Jukwani wakati wa mchezo wa Chelsea dhidi ya Swansea mchezo ambao Chelsea ilishinda 1-0

Be the first to comment

Leave a Reply