Antony Joshua kucheza Nou Camp mapema 2018.

Antony Joshua kucheza na Joseph Parker katika uwanja wa klabu ya Barcelona.

Uwanja wa klabu ya Barcelona wa Nou Camp unaweza kuwa mwenyeji wa mchezo wa masumbwi litakalo wakutanisha wababe Anthony Joshua dhidi ya Joseph Parker, kwa mujibu wa timu ya mapromota Wa New Zealander.

Majadiliano juu ya kuliwezesha pambano hilo la bingwa wa dunia Joshua na Parker yanakaribia kukamilika huku promota wa bingwa wa dunia kutoka Uingereza Eddie Hearn akiwa tumaini mpango kukamilika ndani ya wiki kuanzia sasa na kuwezesha pambano kucheza mwezi Machi au Aprili.

Duco Events ambao wanamuongoza Parker wanaendelea na mchakato wa kupata jukwaa la pambano hilo ukiwemo uwanja wa nyumbani wa Barcelona ambao una uwezo wa kuchukua watazamaji 99,000.

Be the first to comment

Leave a Reply