Arsene Wenger: Sitegemei kumuona Mourinho akipaki basi

Wenger anasema hategemei kumuona Mourinho akipaki basi

Arsene Wenger hategemei kuiona Manchester United ya Jose Mourinho ikilipaki basi wakati Arsenal itakapokuwa mwenyeji Jumamosi katika mfululizo wa michezo ya ligi kuu ya Uingereza.

Timu zote zitakuwa zikiingia katika mchezo huo zikiwa na matokeo ya ushindi katika michezo yao mitatu ya mwisho huku United ikiizidi Arsenal kwa alama 4 na ikikalia nafasi ya pili katika jedwali la msimamo wa ligi hiyo.

United itakuwa ikisaka ushindi wa kwanza katika michezo 8 dhidi ya timu za ‘Top Four’ tangu kuwa chini ya Mourinho, ikiwa imekwenda sare michezo 3 na kufungwa michezo 4 katika michezo 7 ya hivi karibuni lakini pia ikifunga goli moja.

Lakini Wenger anasema hategemei kuona mpinzani wake akiingia katika mchezo huo na mbinu hasi dhidi ya washika mitutu.

Be the first to comment

Leave a Reply