Barcelona kuliamsha tena ‘Dude’ kwa Liverpool kuhusu Coutinho Januari

Barcelona kuliamsha dude kwa Liverpool mwezi Januari kuhusu Coutinho.

Mtendaji mkuu wa klabu ya Barcelona Oscar Grau amesema klabu yake itafanya jaribio lingine tena mwezi Januari kuhusu kumsajili kiungo Philippe Coutinho kutoka Liverpool.

Kigogo hicho cha Katalunya kilishindwa kukamilisha usajili wa nyota huyo wa kimataifa wa Brazil ambaye ni chaguo sahihi la kuziba pengo la Neymar aliyehamia PSG ya Ufaransa.

Coutinho aliwasilisha ombi la kutaka kuondoka Liverpool lakini Liverpool ikigomea mara tatu ofa kutoka Barcelona ambayo iliwasilisha dau la mwisho la paundi milioni 118.

Grau amesisitza klabu yake haijakata tamaa licha ya Liverpool kusalia na msimamo wake wa kumuuza kiungo wake katikati ya msimu.

“tuko tayari kumnunua Coutinho katika soko la majira ya baridi lakini hata kama timu ya ufundi itapendekeza mchezi mwingine” amesema Grau.

Be the first to comment

Leave a Reply