Barcelona kuvunja recodi ya Uingereza endapo itamsajili Coutinho Januari

Liverpool yatangaza dau la mwisho kumuuza Coutinho kwa Barca

MAGAZETI mawili yanaongoza kwa habari za michezo nchini Hispania yameripoti kuwa Liverpool imetajwa bei ya kumuuza kiungo wake Philipe Coutinho ambaye anatakiwa na klabu ya Barcelona.

Sakata la kiungo huyo mshambuliaji raia wa Brazil limechukua nafasi kwa miezi sasa ambalo lilipelekea Barcelona kushindwa kumhamisha mchezaji kutoka Anfield wakati wa dirisha la uhamisho wa wachezaji la kiangazi.

Aidha kwa mujibu wa taarifa hizo nchini Hispania ni kwamba sasa linaweza kufikia mwisho kwani Liverpool inatarajiwa kutangaza dau la mwisho kwa ajili ya kiungo huyo.

Katika ukurasa wake wa kwanza, Mundo Deportivo limesema Coutinho atawagharimu Wakatalunya Euro milioni 145 ambazo ni sawa na paundi milioni 128.

Liverpool ilikataa ofa kwa uchache mara tatu kutoka Barca wakati wa kiangazi na na hivyo watakuwa wakihitaji mzigo mkubwa zaidi kwa ajili ya mchezaji huyo.

Endapo Barca itamsajili Coutinho kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 128, itakuwa ni mara ya kwanza kwa klabu ya Uingereza kuhusika na mpango wa zaidi tarakimu 9 kwa mchezaji.

Be the first to comment

Leave a Reply