Conte alalamikia ratiba ya timu yake

Meneja wa Chelsea Antonio Conte anakerwa na mpangilio wa ratiba ya timu yake

Meneja wa Chelsea Antonio Conte anadai kuwa kuna njama ya mpangilio wa mechi dhidi ya klabu yake.

Conte raia wa Italia awali alinukuliwa akihoji mpangilio wa mechi za ligi ya England kwa kuangazia tofauti ya muda wa kupumzika kati ya klabu yake na wapinzani wake.

Kabla ya mchezo wao wa leo uliopigwa mapema hii leo dhidi ya Newcastle katika uwanja wa Stamford Bridge, kikosi chake kilikuwa na ratiba ya mchezo mmoja mapema wiki hii.

Conte alisema: Ni ngumu kudhani kwamba ni bahati mbaya . Hii ni mara ya nne.

“Iwapo kuna mtu anataka kufanya mzaha nami, basi ajue kwamba mimi sio mtu wa kufanyia mzaha”

Meneja huyo mwenye umri wa miaka 48 hivi majuzi alihoji ni kwa nini kikosi chake kililazimika kucheza dhidi ya Liverpool siku tatu baada ya kuelekea kucheza dhidi ya Qarabag ya Azerbaijan.

Pia amelalamika kuhusu mechi dhidi ya Manchester City na Watford ambazo Chelsea ilicheza baada ya mechi za klabu bingwa Ulaya.

Be the first to comment

Leave a Reply