COSAFA CUP 2016: Madagascar yaanza kwa ushindi dhidi ya Seychelles

Mcolisi Lukhele of Swaziland challenged by Chalton Mashumba of Zimbabwe during the 2016 Cosafa Cup match between Zimbabwe and Swaziland at Sam Nujoma Stadium in Windhoek Namibia on 11 June, 2016 ©Muzi Ntombela/BackpagePix

Madagascar imeanza kwa ushindi dhidi ya Seychelles katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya COSAFA Castle Cup 2016 huku Zimbabwe na Swaziland zikitoka sare ya 2-2.

Madagascar wamewachapa wapinzani wa visiwani na kuanza kuongoza kundi A katika mchezo wa siku ya ufunguzi.

Zimbabwe na Swaziland wakilazimishana sare ya 2-2 katika mchezo ambao Zimbabwe wakilazimika kusawazisha kila mara.

Leo Jumapili kutakuwa na mchezo mwingine ambapo Lesotho watakuwa uwanjani dhidi ya Mauritius katika uwanja wa Independence kabla ya timu ya taifa ya Angola ilisheheni vijana wengi kuumana na Malawi katika uwanja huo.

Angola ni mabingwa mara tatu wa mashinagano ya nchi za kusini mwa bara la Afrika.