Cosmas Cheka asaidiwe kutetea mkanda wake wa Asia-Pasific

Na Ally Kashushu
Bondia Cosmas Cheka ni Mzaliwa wa jijini Dar es Salaam miaka 25 iliyopita.

Ni mototo wa mzee Bonface Cheka ambaye ni mwenyeji wa mkoa wa Mtwara. Cheka amesoma katika shule ya msingi Kinondoni kabla ya kujiunga na shule ya sekondari ya Hananasifu iliyoyoko pia wilayani Kinondoni.

Alinza kungia katika ngumi za kulipwa mwaka 2007 akianzia kambi ya Vijana Social Hall iliyo chini ya kaka yake Fransis Cheka ambaye naye ni bingwa wa uzito wa kati unaotambuliwa na shirikisho la ngumi duniani WBF.

Tangu alipoingia katika ulimwengu wa masumbwi, akicheza kwa kutanguliza mguu mkono wake wa kushoto mbele (Orthodox) Rekodi ya Cheka ni ya kuvutia licha ya kushinda na kushindwa katika mapambano yake ya nyumbani na nje ya nchi ya kushinda mapambano 11 moja nje ya nchi, na kupigwa manne moja pia akipigwa nje ya nchi.

Miongoni mwa mapambano aliyowahi kushinda ni pamoja na kuwachapa wakali kama Deo Njiku,Musa Chiteteteta, Seba Temba, Maneno Chipolopolo, Timo Michael na hata mdogo wake bondia mwingine mkali nchini Mashari Junior.

Kila kilichokizuri hakikosi kasoro, Cosmas Cheka pia amewahi kupoteza michezo yake kadhaa likiwemo pambano lake dhidi ya motto wa bingwa wa zamani Rashidi Mohamed Matumla huyu ni Mohamed Matumla.

Wengine waliowahi kumchapa ni Ramadhani Shauri, Ibrahim Class na lingine huko Namibia, hakika hii ni rekodi ya kupendeza kwake. Baada ya kumchapa Mthailand Thewa Onesongchaigym nchini kwake Thailand Cheka na kuvishwa mkanda wa Asia/ Pasifiki unaotambuliwa na chama cha ngumi za kulipwa WBO, amepata fursa ya kufanya mahojiano maalum na Tamasha la michezo.

Pamoja na ushindi dhidi ya Mthailand, kwa wataalamu wa mchezo wa ngumi watakubaliana na mimi kuwa kuna kila sababu ya kumsaidia kiufundi na kimazoezi Cosmas, kwani katika pambano lake hilo kuna wakati alizidiwa akili na maarifa na mpinzani wake kiasi hata kupoteza mwelekeo hususani raundi ya nne na tano.

Cosmas Cheka alicheza pambano lake na Thewa akiwa na mbinu kidogo sana kujilinda na kuruhusu mpinzani wake licha ya kuwa mfupi kurusha jabu za kutosha na ngumi nyingi za usoni ambazi zilikuwa zikitua sawia kwa Cosmas pengine kama Mthailand angeweza kuwa mvumilivu na pumzi za kutosha basi huenda maamuzi ya raundi 12 za pambano yangekuwa tofauti.

COSMA CHEKA anayefuata nyendo za kaka yake francis cheka amesema kuwa alipatwa na furaha ya aina yake kwa kumchapa Mthailand Thewa kiasi kuangua kilio kwani bondia huyo hakuwa wa kubeza hata kidogo kutokana na kiwango chake cha juu ulingoni.

Aidha anasema kwasasa mabondia wa Tanzania wamuache kwanza kwani anafikiria zaidi mabondia wa nje kwa lengo la kutangaza fani yake na hata kutetea makanda wake.

“kwasasa naomba waniache kwanza ili nipate muda mwingi wa kutetea mkanda wangu”

Pambano la Cosmas nje ya nchi lilisimamiwa na kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini Tanzania PST lililo chini ya Rais Emmanuel Mlundwa aliyeambatana naye Thailand akisadiwa kwa karibu na katibu Antoni Luta.

Mlundwa anasema lilikuwa pambano kali na kwamba uvumilivu na kujituma ulingoni kulikuwa silaha kubwa kwa Cosmas kuweza kumchapa Thewa.

“Pambano lilikuwa gumu nampongeza sana Cosmas kwa uvumilivu wake ulingoni kwakuwa mpinzani wake alikuwa mgumu sana lakini kwa kuwa alikuwa anajua nini anakifanya alifanikiwa kumpiga raundi ya 8 kwa KO”

Mlundwa anawataka mabondia wa Tanzania kujituma zaidi wakati wa maandalizi yao katika michezo yao na hata wanapokuwa ulingoni na kuachana na woga ikiwezekana kuwa wastahamilivu wanapokutana na mpinzani mkali

Kwasasa yuko chini ya makocha Power Iranda,Abdalah Sahele Komando na Pius Ponela GYM ya Vijana Social Hall maeneo ya 77 mjini Morogoro
Tamasha la michezo kwa mara nyingine tena linampongeza kijana huyo kwa kuliletea sifa taifa hili.