Eden Hazard anasema Salah hakupewa nafasi alipokuwa Chelsea

Mohames Salah mfungaji anaeyeongoza ligi kuu ya England msimu huu, amefunga goli 9 katika michezo 12.

Eden Hazard anasema Mohamed Salah hakupewa nafasi ya kujiimarisha alipokuwa Chelsea na kumuelezea mshambuliaji huyo kuwa ni “top, top player”.
Salah alijiunga na Chelsea 2014 lakini aliichezea timu hiyo michezo 19 kabla ya kupelekwa Fiorentina ya Italia kwa mkopo mwaka uliofuata.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 baadaye alihamia AS Roma akiendelea kuhamishwa kwa mkopo kabla ya kukamilisha mkopo huo na kusajiliwa kwa mkataba wa kudumu 2016.
Salah amerejea ligi ya Premier na kujiunga na Liverpool mwezi Julai kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni £34.3 na amekuwa kuwa mfungaji mwenye magoli mengi akifikisha goli 9 katika michezo 12 na Hazard anakiri Salah hakupewa nafasi kuonyesha uwezo wake alipokuwa Chelsea.

Be the first to comment

Leave a Reply