Fellaini na Old Trafford njia panda

Marouane Fellaini ameanza kufikiria hatma yake ya badaye ndani ya Manchester United na akiamini kuwa meneja wake Jose Mourinho kuheshimu uwamuzi wake endapo ataamua kuondoka.

Kiungo huyo ambaye kwasasa ana umri wa miaka 30 atakuwa nje ya muda wake wa mkataba Old Trafford mwisho wa kampeni ya mwaka huu na uwezekana wa kukubali mkataba mwingine unaonekana kuwa mgumu.

Alipoulizwa kama ataendelea kusalia ngome kongwe miezi michache ijayo Fellaini aliambia tovuti ya HUMO ya nchini Ubelgiji “Kiukweli sijui.

“nina kitu kichwani kwangu lakini siwezi kukwambia wewe. Huu ni msimu wangu wa kumi nchini England. Bado nipo hapa, kama Manchester hainihitaji tena wangeniambia muda mrefu, waliweka pendekezo pengine mmoja atalifuata.

Fellaini anaweza kuanza mazungumzo na klabu nyingine mwezi Januari wakati dirisha la uhamisho litakapo funguliwa na anaweza kuihama kuondoka bila kitu chochote akiwa huru mwezi Mei mkataba wake utakapo malizika.

Be the first to comment

Leave a Reply