Ghana yatinga robo fainali kombe la Dunia India

Wachezaji wa Kikosi cha Ghana cha U17 kilichovuka hadi robo fainali sasa kukutana na Mali Jumamosi.

Ghana imewachapa ndugu zao kutoka barani Afrika Niger kwa goli 2-0 katika mchezo wa mtoano hatua ya 16 bora wa mchuano wa kombe la dunia kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 nchi India mchezo uliopigwa Navi Mumbai mapema hii leo. Ushindi huo sasa unawavusha Black Starlets hadi robo fainali na sasa watakutana na waafrika wengine Mali Jumamosi katika dimba la Guwahati.

Ghana ilitawala mchezo katika kipindi cha kwanza na kutengeneza nafasi dhidi ya nafasi moja ya Niger.

Vijana hao kutoka Afrika Magharibi walitengeneza nafasi ya kwanza katika dakika ya 25 kwa shambulizi la nguvu la Edmund Arko-Mensah kabla ya golikipa wa Niger Khaled Lawali.

Iliwabidi Ghana kusubiri hadi dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza kuandika goli la kwanza lililotokana na mpira wa adhabu ya penati baada ya Eric Ayiah kuangushwa ndani ya boksi na Farouk Idrissa. Nahodha huyo wa Ghana alipiga penati hiyo na kuandika goli la kwanza na la tatu kwa upande wake katika mashindano haya.

Black Starlets waliendelea kuliandama lango la Niger baada ya mapumziko huku Gideon Mensah akishindwa kutumia nafasi nzuri ya kuandikisha goli la pili akiwa karibu na goli.

Goli la pili la Ghana limefungwa katika dakika za mwisho baada ya Richard Danso aliyetokea benchi kudhihirisha ubora wake.

Be the first to comment

Leave a Reply