Guardiola aifikia rekodi ya Conte ya tunzo za Premier League

Guardiola ashinda tunzo ya kocha bora wa Premier League mwezi Novemba

Pep Guardiola anakuwa kocha wa pili ndani ya msimu mmoja kushinda tunzo ya kocha bora wa mwezi wa ligi kuu nchini England.

Guardiola anajumlisha tunzo hiyo na zile za mwezi September na October baada ya kukiongoza vema kikosi chake cha Manchester City kushinda michezo 4 ndani ya mwezi huo wa Novemba, na kuifanya ‘Citizens’ kuikaribia rekodi ya ambayo sasa tayari imeifikia ya kushinda michezo 15 mfululizo ambayo ilifikiwa katika mchezo wa ushindi dhidi ya Swansea City Jumatano.

Guardiola raia wa Hispania ameifikia rekodi iliyowekwa na Antonio Conte msimu uliopita ambapo aliifikisha Chelsea kushinda taji la msimu wa 2016/17.

Man City ilizichapa Arsenal, Leicester City, Huddersfield Town na Southampton ndani ya mwezi huo wa Novemba na kumuingiza Guardiola katika orodha ya makocha sita ambao walikuwa wanapambanishwa kuwania tunzo hiyo. Amewashinda Conte, Sean Dyche, Jurgen Klopp, Jose Mourinho na Arsene Wenger.

Be the first to comment

Leave a Reply