Guardiola, Conte, Mourinho, Wenger na Dyche nani kuibuka meneja bora mwezi Novemba?

Premier League imependekeza Guardiola, Conte, Mourinho, Wenger na Dyche kuwani tuzo ya meneja bora wa mwezi Novemba

Pep Guardiola, Antonio Conte, Jose Mourinho, Jurgen Klopp, Arsene Wenger na Sean Dyche wameteuliwa kuwania tuzo ya meneja bora wa mwezi Novemba wa ligi ya Premier.

City ilishinda michezo yote ya mwezi huo dhidi ya Arsenal, Leicester, Huddersfield na Southampton.

Guardiola, ambaye kikosi chake kimeshinda michezo 13 anaweza kulinganishwa na mafanikio ya Conte ya msimu uliopita kwa kushinda tuzo ya meneja bora wa mwezi mara tatu ndani ya msimu mmoja mfululizo.

Conte amekuwa meneja wa kwanza kufanya hivyo baada ya kikosi chake kuwa na ushindi mfululizo michezo 13 na hatimaye akashinda taji la msimu wa 2016/17.

Chelsea ilianza mwezi huo wa Novemba kwa kuichapa Manchester United na kumaliza bola kufungwa kwa kupata ushindi michezo 3 katika michezo 4 ukiwemo mchezo wa sare dhidi ya Liverpool ugenini Anfield.

Kikosi cha Jurgen Klopp cha Liverpool kimeshinda michezo 3 kati ya 4 ndani ya mwezi huo dhidi ya West Ham, Southampton na Stoke.
Burnley pia imekuwa na ushindi wa asilimia 75% ndani mwezi huo baada ya ushindi wa nyumbani dhidi ya Swansea na michezo mingine miwili ya ugenini dhidi ya Southampton na Bournemouth.

Be the first to comment

Leave a Reply