Je Arsenal itaweza kutengeneza rekodi ya Highbury mbele ya Manchester United?

Arsenal itakuwa ikicheza dhidi ya Manchester United ikisaka rekodi ya Highbury Novemba 2005

Arsenal itakuwa ikiwakaribisha wapinzani wao wakubwa Manchester United ikiwa imeshinda michezo 12 mfululizo katika uwanja wake wa nyumbani.

Kwa mara ya mwisho kuwa matokeo kama haya ilikuwa ni kuanzia Februari hadi Novemba 2005 wakati hu ikiutumia uwanja wao wa zamani wa Highbury ambapo ilikamilisha michezo 13 bila kufungwa uwanjani hapo.

Je itaweza kuifikia rekodi hiyo katika dimba la Emirates?

Manchester United itaweza kupunguza mwanya wa alama hadi kufikia 5 kati yake na Manchester City wanao ongoza ligi hiyo wakiwa na alama 40 endapo itashinda katika mchezo huu.

NANI ANAINGIA NANI ANAKOSEKANA KUELEKEA MCHEZO HUU
Mshambuliaji Alexandre Lacazette wa Arsenal ataukosa mchezo huu kufuatia maumivu msuli wa ndani ya paja yaliyotokana na mchezo wa Jumatano dhidi ya Huddersfield.

Alexis Sanchez atakuwepo katika mchezo huu licha ya kubadilishwa katika kipindi cha pili na nafasi yake kuchukuliwa na Danny Welbeck baada ya kuonekana kulalamikia maumivu ya nyama za paja.

Kiungo wa Manchester United Nemanja Matic yuko katika wasiwasi wa kucheza baada kuugulia msuli dhidi ya Watford.

Kiungo mwenzake Marouane Fellaini hatakuwepo katika mchezo kutokana na kusumbuliwa na mguu.
Eric Bailly, Phil Jones na Michael Carrick wote ni wagonjwa na hawatahusika katika kikosi cha Jose Mourinho.

HISTORIA

    Arsenal imefungwa mchezo mmoja tu katika michezo 5 ya mwisho ya ligi kuu ya England dhidi ya Manchester United. Imeshinda mchezo mmoja na kutoka sare michezo miwili.

    Washika mitutu wana dhamira ya kushinda mchezo wa tatu mfululizo dhidi ya United katika uwanja wa nyumbani kwa mara ya kwanza tangu 1991.

    Ushindi wa mwisho wa Manchester United katika dimba la Emirates ulikuwa ni 2-1 November 2014, ulikuwa ni ushindi wa kwanza wa aliyekuwa meneja wa United wakati huo Louis van Gaal katika uwanja wa ugenini.

Be the first to comment

Leave a Reply