Kipa wa Simba Said Mohamed kurejea mapema baada ya upasuaji

Kipa Said Mohamed anaweza kurejea mapema licha ya kufanyiwa upasuaji

Kipa namba mbili wa Simba Said Mohamed, huenda akawahi kurudi uwanjani baada ya tiba ya upasuaji aliyofanyiwa kwenye mguu wake wa kulia kumletea nafuu.
Kwa mujibu wa mtandao wa goal.com Kaimu Makamu wa Rais Idd Kahuna amesema Kipa huyo tayari ameruhusiwa na jopo la madaktari waliomfanyia upasuaji.

“Nikweli wenzetu wa India wametuhakikishia kuwa Said yupo vizuri na Oparesheni imekwenda safi na wameshamruhusu kurudi nyumbani hivyo tunamtegemea muda wowote hapa nyumbani,” amesema Kahuna.

Kiongozi huyo amesema mara baada ya kuwasili nchini Kipa huyo atapatiwa uangalizi wa karibu na daktari wao Yassin Gembe, kabla ya kuanza kucheza.

Amesema kwa mujibu wa madaktari hao wamempa Kipa huyo wiki tatu kabla ya kuanza maisha mapya ya kuichezea timu yake mpya aliyojiunga nayo.

Said hajaichezea Simba takribani mechi zote walizocheza msimu huu kutokana na tatizo la goti ambalo alilipata kwenye mazoezi ya timu ya Taifa

Be the first to comment

Leave a Reply