Kiungo wa Schalke Goretzka awavutanisha Arsenal, Juventus na Barcelona

Leon Goretzka awavuta mashati wakubwa

Manchester United imeungana na klabu nyingine za soka katika mbio za kutaka saini ya kiungo mwenye kipaji wa Schalke Leon Goretzka.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 22 atakuwa nje ya mkataba kiangazi na amepkuwa akitakiwa na klabu yake kuongeza mkataba mwingine wenye masharti mapya.

Aidha, Schalke inakabiliwa na changamoto ya kumshawishi kiungo huyo kusalia Ujerumani.

Arsenal, Juventus na Barcelona zinaonekana tayari zimeanza majadiliano kupitia mawakala wao wakati ambapo Bayern Munich ikiwa tayari imetuma maombi.

Meneja wa United Jose Mourinho anataka kuimarisha kiungo chake wakati Michael Carrick akiwa anaelekea ukiongoni kama ilivyo kwa Henrikh Mkhitaryan na Juan Mata ambao wana kazi kubwa ya kufanya kumshawishi Mourinho kuwa wanavitu vya ziada.

Goretzka anafiti mahitajio ya Mourinho kuwa na kiungo mwenye urefu wa futi sita na nchi mbili. Anaweza kucheza chini na karibu na boksi la wapinzani akingia na kutoka na tayari ameshafunga goli katika michezo ya kimataifa akiwa na kikosi cha Ujerumani.

Be the first to comment

Leave a Reply