Kocha Fransis John wa Tanzania ana matumaini na Medali Olimpiki

Wachezaji wa nne wa timu ya taifa ya Tanzania wataokwenda kushirikia michuano ya olimpic.Wanaendelea na maandalizi ya mwisho katika kambi yao iliyoko West Kilimanjaro huko mkoani Kilimanjaro kabla ya kuelekea nchini Brazil kushiriki michuano ya Olimpic.

Tanzania itawakilishwa na wanariadha wanne katika michuano hiyo, ambao ni Alponce Felix, Fabiani Joseph, Saidi Juma pamoja na Sara Ramadhani.

Kocha wa kikosi hicho Francis John anasema ” wamekaa miezi saba kambini wakijiandaa na michezo hiyo mikubwa hivyo wanamatumaini makubwa watafanya vizuri na kurudi na medali.

Michezo ya olimpic itaanza kutimu vumbi kuanzia tarehe 5 Agosti na kufikia tamati Agosti 21,kwa jumla ya mataifa 207 yakishirishiki katika matukio 306 ya michezo 28 tofauti .”