Kuhusu Rockersports

Imezinduliwa na Mwandishi na mtangazaji anaelekea kuwa mkongwe wa habari za michezo na burudani nchini Tanzania Ally Kashushu, Rockersports tovuti ya habari za michezo na burudani kitaifa na kimataifa ikiwa ni kwa lengo la kukata kiu ya habari za habari ikiwa ni pamoja na uandishi wa makala na uchambuzi kuhusu michezo na wanamichezo.

Rockersports ilianzishwa mwaka 2008 kama rockerports.blogspot.com, kabla ya kubadilika na kuwa tovuti kamili na sasa ni rockersports.co.tz ikiwa ni kwa lengo la kutengeneza uwanja mpana zaidi wa utoaji wa habari kwa wasomaji wake ndani na nje ya nchi.

Tovuti hii imejikita zaidi kuandika habari za kweli na si za kusadikika kwa kufuata uweledi wa tasnia ya habari ikiwa ni pamoja habari za kichunguzi, habari za kuvunjika(breaking news) habari za muendelezo, na hata zile za moja kwa moja(live events) uchambuzi wa kitaalamu, maoni ya mwandishi na wadau kwa kuangalia faida ya msomaji wetu na kumtengenezea upeo mpana wa michezo na burudani.

Rockersports ni mtandao wenye lengo la kukuhabarisha kwa masaa 24 bila kuchoka kwa huku waandishi wenye uweledi wakifanya kazi hiyo kwa kufuata uweledi na kwa kuzingatia hitajio la jamii nzima. Tunahamu kubwa ya kukupeleka msomaji wetu katika eneo lingine la habari mtandaoni hivyo usikose kupita kila siku kwa habari za kutosha na kusisimua.

Rockersports ni zao la kampuni ya Rockers Media Group(RMG) ambayo inafanya shughuli mbalimbali za habari ikiwemo matangazo, matukio ya moja kwa moja sambamba na promosheni mbalimbali za burudani.

Be the first to comment

Leave a Reply