Ligi kuu ya England inaelekea wiki ya 16, kuna ‘dabi’ mbili za Merseyside na Manchester nini kinakwenda kutokea?

Wiki ya 16 ya ligi kuu ya Uingereza kuna dabi mbili kubwa pale katika jiji la Manchester ni United dhidi ya City na Mersyside ni Liverpool dhidi ya Everton.

Wikiendi hii ligi kuu ya nchini England itakuwa inaingia katika wiki ya 16 huku kila upande ukijaribu kusaka alama 3 muhimu na kujiweka vizuri katika jedwali la msimamo wa ligi.

Wakati Liverpool na Everton zikikutana katika Derby ya Merseyside Jumapili katika dimba la Anfield. Katika jiji la Manchester kutakuwa na Derby nyingine Manchester United watakapokuwa wakiwakaribisha Manchester City.

MARSEYSIDE DERBY
LIVERPOOL VS EVERTON

Wekundu wa Liverpool hawajafungwa katika michezo yote 14 ya mwisho dhidi ya wapinzani wao wa jiji katika mashindano yote, isipokuwa katika kumbukumbu kuna mchezo mmoja pungufu dhidi ya wapinzani hawa wa Merseyside 15), ambao ulipangwa kuchezwa Machi 1972 na Aprili 1978.

Ingawa kiwango cha Everton kiliongezeka ubora katika wiki zilizopita ambapo ilishinda na kutunza ‘Clean Sheets’ katika michezo miwili ya mwisho ya ligi kuu, bado haijafanikiwa kushinda katika michezo 17 ya ligi pale inapotembelea Anfield (D8 L9) tangu iliposhinda mara ya mwisho Septemba 1999 goli lililofungwa na Kevin Campbell.

Liverpool haitaingia katika ‘Merseyside Derby’ ikiwa haijafungwa katika michezo 9 ya mwisho ya mashindano mbalimbali na imekuwa ikifunga idadi kubwa ya magoli ambapo katika idadi hiyo ya michezo jumla ya goli 32 zimefungwa ikiwa ni wastani wa goli 3 katika kila mchezo. Magoli saba kati ya hayo yamefungwa katikati ya wiki katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi michuano ya klabu bingwa Ulaya ambapo iliichapa CSKA Moscow goli 7-0 katika dimba la Anfield – Hiyo imefanya kuwa ni mara ya pili kufunga goli saba katika hatua ya makundi msimu huu.

Kuna hali ya hewa chanya inaitambalia Everton hivi sasa kwani imefanikisha ushindi wa ‘Back-to-Back’ tangu alipotangazwa Sam Allardyce kuwa kocha meneja mpya wa kikosi hicho wenyeji wa Goodison Park. ‘Big Sam’ alikuwa akiangalia mchezo wa ushindi wa goli 4-0 dhidi ya West Ham United saa moja baada ya kutangazwa kuwa meneja mpya na alianza kukalia mikoba ya benchi la ufundi kwa mara ya kwanza akafanikiwa kupata ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Huddersfield Town.

Bila shaka dhamira na mawazo ya Allardyce kwasasa ni kuona kikosi chake kinapata ushindi mwingine wa tatu katika mchezo huu wa Merseyside Derby ambayo kwake ni ya kwanza, Je atafanikiwa? Bila shaka alikuwa na maamuzi chanya alipoingia katika mchezo wa katikati ya wiki wa michuano ya Europa kule Cyprus dhidi ya Apollon Limassol, akiwapumzisha wachezaji wake muhimu kwa ajili ya mchezo huu dhidi ya Liverpool.

MANCHESTER DERBY
MANCHESTER UNITED VS MANCHESTER CITY

Inawekuwa kuwa pekee katika mwezi Desemba lakini mchezo huu mkubwa wa Jumapili kati ya Manchester United na Manchester City unaweza kuwa mwamuzi katika mbio za ubingwa ligi msimu huu wa 2017/2018. Endapo United itaifunga City basi itakuwa ni klabu ya kwanza katika ligi ya nyumbani kuishinda City msimu huu lakini si hivyo tu itaweza pia kupunguza mwanya wa alama kati ya timu hizi mbili, lakini endapo kikosi cha meneja Pep Guardiola kitaibuka na ushindi Old Trafford kitazidi kutanua mwanya wa alama hadi kufikia 11 kileleni. Kinachosubiriwa ni namna gani hilo litafanyika?

Katika wakati fulani United imekuwa ikitereza msimu huu, lakini wakati fulani imekuwa ikionyesha kutoa changamoto katika mbio za ubingwa. Ushindi wa wikiendi iliyopita wa goli 3-1 ugenini dhidi ya Arsenal imetoa mwanzo mwingine mzuri katika mbio hizi kwani imeweza kufikisha ushindi wa michezo 4 mfululizo huku kiwango cha golikipa David De Gea katika mchezo huo kilikuwa bora sana na kuchagiza muelekeo mzuri wa kikosi hicho. Raia huyo wa Hispania kwa mara nyingine aliamsha mjadala wa kuwa anaweza kuwa golikipa bora duniani na mashetani wekundu kuonyesha kuhitaji kuona ubora wake huo katika mchezo huu dhidi ya timu yenye safu bora ya ushambuliaji.

Manchester City imekuwa haikamatiki msimu huu. Ilipoteza muelekea katika mchezo wa katikati ya wiki pale ilipofungwa na Shakhtar Donetsk katika mchezo wa klabu bingwa Ulaya ambapo walifungwa 2-1. Tayari vinara hao wa ligi kuu ya England walikwisha kukata tiketi ya hatua ya makundi ya ligi hiyo ya vilabu Ulaya na kuelekea mchezo huu dhidi ya United meneja wake Guardiola alitoa mapumziko kwa baadhi ya wachezaji wake. Kama kikosi hicho kinapangwa kamili kila idara kinakuwa hakishikiki msimu huu.

Tayari kimekusanya alama 43 katika uwezekano wa alama 45 za ligi kuu ya England na rekodi yake ya ugenini inasomeka vizuri kwani kimeshinda michezo yote saba ya ugenini.

Lakini kwa upande wa pili, Manchester United imekuwa bora sana katika uwanja wake wa Old Trafford. Imeshinda michezo yote ya kimashindano wakicheza ndani ya ‘Theatre of Dreams’ hadi sasa msimu huu, na katika ligi kuu imefunga goli 20 na kuruhusu goli moja kitu ambacho kinaifanya kuwa rekodi iliyotukuka. Hii maana yake kuna kitu cha kufanya hapa lakini swali linabaki kuwa itaweza kutunza rekodi hiyo ya asilimia 100 nyumbani au City inatunza rekodi yake ya ushindi ugenini kwa asilimia hizo?

Hii ni Derby ya kwanza kwa timu hizi zikiwa katika nafasi mbili za juu katika jedwali la msimamo wa ligi tangu April 2013.

West Ham United vs Watford
London Stadium

Mbali na michezo hiyo hiyo miwili wikiendi hii, kule katika dimba London, West Ham watakuwa wenyeji wa Mabingwa watetezi Chelsea
Chelsea imepoteza michezo miwili tu katika michezo 22 ya mwisho ya ligi ya Premier dhidi ya West Ham United ambapo imeshinda michezo 16 na kwenda sare michezo 4 ikishinda michezo yote miwili ya msimu uliopita kwa goli 2-1.

West Ham United itataka kupata ushindi wa kwanza baada ya kwenda mchezo 8 ya mwisho bila ushindi ikitoka sare michezo 3 na kufungwa michezo 5 yakiwa ni matokeo mabovu kwao tangu Decemba 2015.

David Moyes ameshinda michezo 4 ya mwisho katika michezo 5 ya mwisho katika uwanja wa nyumbani dhidi ya timu bingwa mtetezi akiwafunga mara tatu mameneja wa Italia ambao wamekuwa watetezi wa mataji wakiwemo Carlo Ancelotti, Roberto Mancini na Claudio Ranieri.

Eden Hazard yuko katika fomu na kuelekea katika mchezo huu atakuwa akitarajia kuidhoofisha idara ya ulinzi ya West Ham ambayo imefungwa goli nyingi zaidi kuliko timu zote msimu huu.

Burnley vs Watford
Turf Moor Stadium

Timu hizi mbili zimekuwa na mafanikio zaidi katika msimu huu wa 2017/18, hivyo mchezo huu utakuwa ni fursa kwa kila upande kuweza kurudisha changamoto katika eneo la Top 6 la msimamo wa.

Burnley ilishuka hadi nafasi ya 7 baada ya kichapo cha 2-1 kutoka kwa Leicester City.

Watford iko katika nafasi ya 8 ikiachwa kwa alama 3 na wapinzani wao wa wikiendi hii, ilitereza katika michezo miwili iliyopita ambapo ilichapwa 4-2 na Man United wikiendi iliyopita ikatoka sare ya 1-1 Spurs.

Burnley itakuwa na faida ya uwanja wa nyumbani na hivyo matokeo ya sare yatakuwa na faida kwa Watford.
Kule Selhast Park, Crystal Palace itakuwa mwenyeji wa Bournemouth.

Wiki iliyopita Crystal Palace alipanda hadi nafasi ya 18 katika jedwali la msimamo wa ligi hiyo na hiyo ilitokana na kwenda sare michezo 3 na kushinda mchezo mmoja katika mchezo 4 ya mwisho ikiwemo michezo miwili ilimalizika kwa suluhu dhidi ya Brighton na West Brom.

Bournemouth ipo katika nafasi ya 14 kufuatia kushinda michezo 4 na kwenda sare michezo 3, katika michezo mitatu ya mwisho, timu hiyo imekwenda sare katika michezo dhidi ya Swansea na Southampton na kufungwa na Burnley.

Palace bado haijafanikiwa kuifunga AFC Bournemouth ndani ya dimba la Selhurst Park katika michezo ya ligi ambapo mchezo wa mwisho kushinda ulikuwa April 1988.

Huddlesfield vs Brighton & Hove Albion
John Smith Stadium

Huddersfield imeporomoka hadi katika nafasi ya 16 baada ya matokeo ya ushindi michezo 4 sare 3 na vichapo 8 huku na hivi karibuni ikichapwa mfululizo na Bournemouth, Man City, Arsenal na Everton ambapo katika michezo hiyo imeruhusu nyavu zake kutikiswa mara 13 na yenyewe kufunga goli moja.

Brighton imetereza hadi nafasi ya 12 baada ya kushinda michezo 4 sare 5 na vichapo 6 na katika michezo 4 iliyopita imefungwa mara mbili na kutoka sare michezo 2 kikiwepo kichapo cha goli 5-1 kutoka kwa Liverpool wiki iliyopita.

Timu hizi zote zitakuwa zinakutana kwa mara ya kwanza katika ligi kuu na zitakuwa zikiwategemea nyota wao Aussie stars, Mat Ryan na Aaron Mooy, wakati wakijaribu kubadilisha hali ya matokeo katika mwezi huu mgumu katika ligi ya Premier.

Anthony Knockaert atakuwa akiingia katika mchezo huu akiwa anahusika katika magoli 8 dhidi ya Huddersfield katika mashindano yote ikifunga goli 5 na kutoa pasi za mwisho 3.

Swansea vs West Bromich Albion
Liberty Stadium

Kule Wales katika dimba la Liberty Swansea itakuwa tayari kuikabili West Bromich Albion ikiwa ni vita dhidi ya timu mbili zinazo gaa gaa katika upwa wa ukanda wa kushuka daraja.

Swansea iliyoshinda michezo miwili na sare tatu, sasa inazibeba timu nyingine zote 19 katika jedwali la msimamo wa ligi hali hiyo imechagizwa na timu hiyo kuambulia alama moja tu katika michezo 7 ya karibuni, katika mchezo wa mwisho ikidondoshwa na Stoke 2-1.

West Brom kwasasa iko katika nafasi 17 ikiwa ni alama 3 juu ya timu zilizo chini ya mstari wa kushuka daraja. Imekwenda sare tatu mfululizo dhidi ya Spurs, Newcastle na Palace baada ya kumaliza mfululizo wa vichapo 4. Itakumbukwa West Brom haijashinda tangu wiki ya pili ya ligi hii.

Swansea imeshinda michezo yote mitatu ya mwisho katika uwanja wake wa nyumbani ikifunga goli 6 na kufungwa moja.
Mlinzi wa Swansea Federico Fernandez atakuwa akirejea kikosini baada ya kukosekana katika michezo mitatu ya mwisho baada ya kufiwa na baba yake.

Newcastle vs Leicester City
West Bromich Albion Stadium

Katika uwanja wa West Bromich Albion, Newcastle United watakuwa wakitifuana na Leicester City.

Newcastle imezidi kimatokeo kushuka hadi nafasi ya 15 baada ya kuambulia alama moja katika michezo yao 6 ya mwisho, baada ya sare dhidi ya West Brom na kichapo cha 3-1 ugenini dhidi ya Chelsea wikiendi iliyopita.

Leicester iko katika nafasi ya 9 katika jedwali baada ya kuandikisha rekodi ya kushinda michezo 5 sare 5 na kufungwa michezo 5 huku katika michezo yao miwili ya mwisho ikipachomza na ushindi dhidi ya Tottenham na Burnley.

Kikosi hicho cha meneja Claud Puel kimefungwa mchezo mmoja tu katika michezo 9 ya mwisho.

Leicester imekuwa katika mtiririko bora wa ushindi dhidi ya Newcastle. Endapo Jamie Vardy atafunga katika mchezo huu atakuwa ni mchezaji wa kwanza wa Leicester kuifikia idadi ya magoli 50 ya ligi ya Premier.

Be the first to comment

Leave a Reply