Maandalizi ya michuano ya CHAN kufanyika Novemba 12 Rabat

Morocco itakuwa mwenyeji wa michuano ya CHAN badala ya Kenya iliyonyang'anywa uwenyeji.

Hafla ya upangaji wa ratiba ya michuano ya 5 ya mataifa ya Afrika nchini Morocco 2018 itafanyika Ijumaa ya Novemba 17 2017 mjini Rabat nchini Morocco.

Michuano hiyo imepangwa kuanza Januari 12 na kumalizika Februati 4 nchini 2018 nchini Morocco katika miji ya Agadir, Casablanca, Marrakech na Tangier ambayo itajumuisha mataifa 16 na kushirikisha wachezaji wanaocheza soka ndani ya nchi zao.

Mkutano wa kamati ya ndani ya maandalizi ya michuano hiyo itakayodhaminiwa na kampuni ya mafuta ya Total, utafanyika Novemba 15 mjini Rabat, na kuamua utaratibu wa upangaji wa ratiba.

Mshindi wa mara ya mwisho Jamhuri ya Demokrasia ya Congo aliyeshinda taji hilo nchini Rwanda, hatatetea taji hilo kufuatia kuondolea na majirani zao Congo katika michezo ya kufuzu.

Nchi zilizofuzu ni Morocco (nchi mwenyeji)
– Egypt, Libya (Kanda ya Kaskazini)
– Uganda, Sudan (Kati na Mashariki)
– Cameroon, Congo, Equatorial Guinea (kanda ya kati)
– Guinea, Mauritania (Kanda A magharibi)
– Burkina Faso, Côte d’Ivoire, Nigeria (Kanda B magharibi)
– Angola, Namibia, Zambia (Kanda ya kusini)

Be the first to comment

Leave a Reply