Manchester City yanogewa na Sterling

Manchester City kufungua mazungumzo na Raheem Sterling juu ya kuongeza muda mkataba wake Etihad.

Manchester City imefungua mazungumzo na mfungaji anayeongoza ndani ya klabu hiyo Raheem Sterling juu ya mkataba mpya.

Winga huyo wa kimataifa wa England amekuwa katika kiwango cha kusisimua msimu huu akiwa tayari amefunga goli 13 katika michezo 19 aliyoshuka dimbani.

Sterling bado ana miaka miwili na nusu ya mkataba wake na City lakini klabu hiyo imesema ina dhamira ya kufungua mazungumzo mapya ya winga huyo.

City haijatoa muda maalumu ni lini mazungumzo hayo yataanza. Sterling alifunga goli muhimu la ushindi dakika ya 96 dhidi ya Southampton Jumatano.

Sterling alijiunga na City akitokea Liverpool Julai 2015 uhamisho uliongarimu paundi milioni 49, na tangu wakati huo ameifungia timu hiyo goli 34 katika michezo 113 aliyocheza.

Be the first to comment

Leave a Reply