Manchester United: Smalling na Phil Jones nje kwa muda usiojulikana

Walinzi Chris Smalling na Phil Jones wamepata majeraha ambayo yatawaweka nje ya uwanja kwa muda mrefu majeraha waliyopata walipokuwa katika majukumu ya kimataifa, amesema meneja wa Manchester United, Jose Mourinho.

Jones mwenye umri wa miaka 25, amepata majeraha ya mputa wa wa kidole cha mguu alipokuwa mazoezi baada ya kukabiliana na Smalling.

Mwenzake mlinzi wa kati Smalling mwenye umri wa miaka 27 alionekana katika picha akiwa na vifaa vya kumsaidia kutembea (leg brace) baada ya kuumia akiwa mazoezini.

Mlinzi Axel Tuanzebe mwenye umri wa miaka 19, ambaye ameitumikia United mchezo mmoja yumo katika orodha ya kikosi cha mashetani wekundu kitakachoikabili West Brom hapo kesho.

United pia itamkosa mshambuliaji wake muhimu Zlatan Ibrahimovic na kiungo Ander Herrera, ambao wote kwa pamoja wanatumikia adhabu ya kusimama michezo kadhaa wakati ambapo kiungo wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba akiendelea kuuguza nyama za paja.

Alipoulizwa itachukua muda gani kabla ya wachezaji Jones na Smalling kurejea katika hali zao za kawaida bosi huyo wa United alijibu “sijui,sijui”.

“ninachojua ni kwamba Zlatan na Herrera wanamalizia adhabu ya kusimamishwa, hivyo ni rahisi kusema watakuwa katika kikosi baada ya mchezo huu.

“nadhani vijana hawa waingereza ni majeruhi wa muda mrefu na Pogba sina uhakika, sijui .”