Mkimbiza upepo Usain Bolt sasa kujiunga na Dortmund ya Ujerumani

Klabu ya Ujerumani ya Borussia Dortmund imesema kuwa mwanariadha wa mbio fupi kutoka Jamaica Usain Bolt atashiriki mazoezi na klabu hiyo kwa siku chache.

Bolt amekuwa akisema kwamba angependa kucheza soka baada ya kustaafu katika riadha.

Lakini wakimkaribisha, maafisa wa klabu hiyo wamesema kuwa hakuna hakiksho kwamba mwanariadha huyo ataichezea klabu hiyo katika siku za usoni.