Mo Salah: ‘Mwaka 2017 umejibu ndoto zangu’

Salah amewashinda Sadio Mane na Pierre-Emerick Aubameyang

Mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri Mohamed Salah amesema mwaka 2017 ulikuwa ni mwaka wa aina yake kwake kwani umegeuza ndoto zake kuwa kweli.
Ametoa kauli hiyo kufuatia kutangazwa kwake kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika katika hafla ya utoaji tunzo iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Accra nchini Ghana usiku wa jana.
Salah alikuwa akishindana na Pierre-Emerick Aubameyang, na Sadio Mane na akaibuka bora zaidi kwa wingi wa kura na ubora awapo kiwanjani.

Kabla ya kujiunga na Liverpool alikuwa katika kikosi cha Roma ya Italia ambako pia alikuwa katika kiwango cha dunia
Ameshinda tunzo baada ya kupigiwa kura 625 kutokana na kucheza michezo 57 ndani ya mwaka huo ambapo amefunga magoli 36, huku nyota mwenzie wa Liverpool Sadio Mane aliyeshika nafasi ya pili akipigiwa kura 507 kufuatia kucheza michezo 36 na kufunga magoli 16. Mshindi wa tatu Pierre-Emerick Aubameyang wa Dotmund amepigiwa kura 311 kutokana na michezo 51 lakini akifunga goli 43.
Salah ametwaa tuzo hiyo kwa mara ya kwanza maishani mwake na anakuwa mchezaji wa pili kutoka nchini Misri baada ya Mahmoud Al Khatib aliyeshinda mwaka 1983.
‘ndoto yangu imetimia. 2017 ulikuwa ni kwaka ambao siamini macho yangu kwa timu ya taifa na klabu yangu’ hayo ni maneno ya Salah baada ya kutangazwa mshindi.
‘kutinga kombe la dunia baada ya miaka 28 kwa taifa langu na ubora wangu katika vilabu vya Roma na Liverpool ni wakati wa kipekee katika kazi yangu.’

Be the first to comment

Leave a Reply