Mshabiki wa liverpool wachoma Jezi ya Coutinho

Taarifa za Coutinho kuihama Liverpool zimewakera mashabiki wa klabu hiyo na kuamua kuchoma jezi ya kiungo huyo raia wa Brazil.


Hatimaye Philippe Coutinho amekamilisha uhamisho wa kujiunga na Barcelona kwa ada ya uhamsho ya paundi milioni 145 akitokea Liverpool.

kiungo huyo raia wa Brazil ameelekea Hispania akitokea London Jumamosi jioni kumalizia hatua za mwisho za kukamilisha mpango huo.

Coutinho alikuwa na Euro milioni 400 (sawa na paundi milioni 355) zinazo jumuisha kuvunjwa kwa mkataba wake kabla ya kuingia kandarasi ya miaka mitano na nusu ya kuichezea Barcelona.

Katika hatua nyingine
Mashabiki wa Liverpool wamechoma moto jezi ya aliyekuwa kiungo wao Philippe Coutinho kabla ya kuihama klabu hiyo.

Nyota huyo raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 25 alikuwa akihusishwa na kuelekea Barcelona na anaweza kukamilisha uhamisho wa kuelekea Barcelona muda wowote kuanzia sasa.

Barcelona ilishindwa mara tatu kumsajili kiungo huyo wakati wa uhamisho wa kiangazi iliyopita huku jaribio lao la mwisho likiwekewa dau la paundi milioni 114.

Aidha klabu hiyo ya Nou Camp sasa imeweka nyongeza ya paundi milioni 130 ili kufikia lengo la kumsajili Coutinho.

Coutinho akipanda ndege yake kutoka London kuelekea Barcelona kukamilisha mpango wa uhamisho wake wa kuichezea klabu hiyo kwa mkataba wa miaka mitano na nusu dili lililokamilishwa kwa ada paundi milioni 145.

Be the first to comment

Leave a Reply