Musonye atoa povu Zimbabwe kujitoa chalenji

Katibu wa CECAFA Musonye amelikanya shirikisho la soka la Zimbabwe ZIFA kufuatia kujitoa kwao katika michuano ya Chalenji.

KATIBU mkuu wa baraza la vyama vya soka Afrika mashariki na Kati (CECAFA) Nicholas Musonye amelilalamikia shirikisho la soka la Zimbabwe (ZIFA) kwa kutangaza kujitoa kushiriki michuano ya kombe la Chalenji wakiwa kama timu alikwa.

Musonye alikusanya waandishi wa habari nje ya mkutano wa kutangaza makundi na ratiba ya michuano hiyo itakayo anza tarehe 3/12/2017 na kusema sababu iliyotolewa na ZIFA hazina msingi kuwa hali ya usalama si shwari nchini Kenya huku wakijua kuwa hali ni mbaya zaidi nchini kwao.

Jumatano ZIFA ilitangaza kujitoa kwa madai hali kutokuwa ya utulivu nchini Kenya kufuatia uchaguzi mkuu wa hivi karibuni.

Zimbabwe amewataka ZIFA kuziba midomo yao kama walikuwa hawana nia ya kweli ya kushiriki michuano ya Chalenji na kuongeza kuwa wao wana matatizo yao hivyo hawapaswi kuzungumzia hali ya usalama nchini Kenya.

“Zimbabwe inapaswa kukaa kimya kama walikuwa hawataki kushiriki, wao wana matatizo yao makubwa kuliko ya kwetu hawawezi kuzungumzia usalama ndani ya Kenya”.

“waliomba kushiriki na tukawafikiria, hatukuwa na ulazima wa kuwaalika (Zimbabwe) hivyo tunasonga mbele” Ameongeza

Pia Musonye amethibitisha timu ntingine mwalikwa ya Libya, itawasili nchini Kenya Jumamosi.

Uganda Cranes ndio mabingwa watetezi baada ya kushinda tajilo mwaka 2015 nchini Ethiopia.

Be the first to comment

Leave a Reply