Nadal kuikosa michuano ya Basel

Maumivu kumnyima nafasi Rafael Nadal michuano ya Basel.

Mchezaji namba moja kwa ubora duniani Rafael Nadal atakosekana katika michuano ya Basel kutokana na majeraha ya goti.

Nadal mwenye miaka 31 amesema kutokana na maumivu hayo ameshauriwa na madaktari wake kupumzika.

Alipata majeraha hayo alipocheza katika fainali za Shanghai Masters dhidi ya Roger Federer aliyeibuka mshindi.

”Ni muda wa kupumzika,” alisema Nadal ambaye ameshinda mataji sita msimu huu akicheza michezo 75.

Kukosekana kwake kunatajwa kwamba kutamfanya Federer kutamba katika michuano hiyo.

Nadal alirejea katika nafasi ya kwanza duniani mwaka 2014 baada ya kushindwa kupata nafasi hiyo kwa muda mrefu kutokana na kuandamwa na majereha mara kwa mara.

Be the first to comment

Leave a Reply