Paul Clement kumsajili nahodha wa Chelsea Terry kiangazi

Paul Clement ameonyesha nia ya kumsajili nahodha wa Chelsea John Terry kiangazi kama Swansea itapona kutoka kwenye janga la kushuka daraja la ligi ya Premier.
Clement amekuwa akifahamiana na Terry tangu alipokuwa naye Stamford Bridge, wakati huo meneja huyo wa sasa wa Swansea akiwa msaidizi wa Carlo Ancelotti ambapo walifanikiwa kushinda taji la ligi ya Premier msimu wa 2009-10.
Clement amejibu tangazo la Terry la kuihama Chelsea mwisho wa msimu na kusema angependelea kumpelekea mlinzi huyo mkongwe Wales Kusini.
Clement aliwahi kufanya jaribio la usajili kwa nyota wa zamani wa Blues, Frank Lampard mwezi Januari kabla ya kiungo huyo wa zamani wa England kutangaza kustaafu.
Hata hivyo Clement amekubali kuwa nafasi pekee ya Swansea kufanikiwa kumsajili Terry ni kuepuka kushuka daraja mpango ambao atakuwa akiendelea nao katika mchezo wa hapo kesho dhidi ya Stoke.

ZLATAN IBRAHIMOVICH NA MARCOS ROHO WAINGIA ORODHA YA MAJERUHI uNITEDzlatan
Mshambuliaji anayeongoza kwa kutupia kambani katika klabu ya Manchester United, Zlatan Ibrahimovic na mlinzi Marcos Rojo wameingia katika orodha ya wachezaji majeruhi ya klabu hiyo yalitokana na mchezo wa robo fainali ya michuano ya Europa dhidi ya Anderlecht.
Ibrahimovic amekutana na maswahibu hayo alipokuwa katika harakati za kuwani mpira ilhali Rojo aliyelazimika kutolewa nje katika dakika ya 27 ya mchezo, yeye aligongana na mlinzi wa timu ya Anderlecht
Bosi wa United Jose Mourinho amesema taarifa za majeraha kwa wachezaji hao ni mbaya kwa mustakabali wa kikosi hicho.
Ibrahimovic, ambaye amefunga goli 28 msimu huu tangu kuwasili kwake kama mchezaji huru akitokea Paris St-Germain kiangazi bado hajakubaliana na matakwa ya klabu hiyo ya kuongeza mkataba kwa kipindi kingine cha mwaka mmoja.
Majeraha kwa Rojo yana maana kuwa sasa anaungana na walinzi wengine Chris Smalling na Phil Jones katika orodha ya wachezaji wa klabu hiyo walio majeruhi.

TOBY ALDERWEIRELD AHUSISHWA NA KUELEKEA iNTER MILAN
Na Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino anasisitiza hasumbuliwi na ripoti ya mlinzi wake Toby Alderweireld kuihama klabu hiyo.toby
Mlinzi huyo wa kimataifa wa ubelgiji amekuwa akihusishwa na kutaka kujiunga na Inter Milan inayoshiriki ligi ya Serie A ambayo imejidhatiti kutoa kitita mwisho wa msimu ikiwa chini ya wamiliki wa klabu huiyo Suning Group.
Ripoti kupitia Sky Italia imesema Nerazzurri wako tayari kufikia kiwango cha ada ya uhamisho ya paundi milioni 25 ili kuweza kuvunja mkataba wa Alderweireld, taarifa ambayo haimshitui Pochettino.

Share and Enjoy

Be the first to comment

Leave a Reply