Pep Guardiola: Tuna kikosi kizuri na kipana kukabiliana na ratiba za siku za sikukuu

Pep Guardiola anajivunia ukubwa wa kikosi chake kukabiliana na ratiba za michezo ya siku za sikukuu

Pep Guardiola anadhani kikosi chake cha Manchester City ni imara kukabiliana na ratiba ndefu ya kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka.

Guardiola haamini kikosi hicho kuchoka wakati wakipambana na ratiba ya michezo ya ligi ya nyumbani na Ulaya.

Alipoulizwa kama kuna uwezekano wa ‘fatigue’ kuingia kikosini punde, Guardiola ameuambia mtandao wa klabu yake kuwa “sidhani hivyo. Pengine itatokea lakini tuna kikosi kizuri cha kutosha.”

Be the first to comment

Leave a Reply