Pogba: Tunaweza kuifunga Manchester City Jumapili

Paul Pogba ana matumaini ya kuifunga Manchester City mchezo wa wikiendi hii

Paul Pogba ana matumaini kikosi cha Manchester United kinaweza kuichapa Manchester City Jumapili na kumaliza matumaini ya Citizens kuweka rekodi mpya ya ligi ya Premier msimu huu.

United itakuwa mwenyeji wa City baada ya mchezo wa Derby ya Merseyside kati ya Liverpool na Everton huku kikosi cha Pep Guardiola kikijipanga kuweka rekodi mpya ya ligi ya kushinda michezo 14 mfululizo endapo itashinda Old Trafford.

Pogba hatakuwepo katika mchezo kufuatia kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo uliopita wa ligi dhidi ya Arsenal Jumamosi iliyopita, huku United ikiachana na rufaa ya adhabu hiyo ya Pogba ya kusimama michezo mitatu.

Pogba anasema pamoja na kuukosa mchezo huo lakini imani yake ni kubwa United itachomoza na alama zote tatu dhidi ya vinara hao wa jedwali la msimamo wa ligi.

Be the first to comment

Leave a Reply