RAIS WA TFF AZUNGUMZA NA WAHARIRI WA HABARI

SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
TAARIFA YA DIRA NA MUELEKEO WA TFF
ILANI YA UCHAGUZI YA RAIS KARIA (First XI ya Karia)
KIKAO CHA RAIS WA TFF BWANA WALLACE KARIA NA
WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI ZA MICHEZO NCHINI
Tarehe 27/12/2017, SEASCAPE HOTEL, DAR ES SALAAM
1.0 SHUKRANI.
Ndugu Wahariri nikizungumza nanyi mkiwakilisha wadau wetu
wote wa Mpira wa Miguu Tanzania, mazungumzo yangu leo
Naomba yaanze kwa Shukrani:
 Naanza kwa Kumshukuru MwenyeziMungu anayetuwezesha
sote kufanya shughuli zetu
 Naishukuru Familia yangu,
 Nawashukuru Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF kwa
Imani yao kwangu na kunichagua kwa kishindo kuwa Rais
wa TFF,
 Naishukuru Serikali ya Jamhuri Ya Muungano wa TANZANIA
inayoongozwa na Mh Rais John Pombe Magufuli kwa
Ushirikiano mkubwa TFF inaopata kutoka kwake
 Naishukuru binafsi pia Serikali ya Mkoa wa Dar es salaam
yalipo Makao Makuu ya TFF kwa ushirikiano wao nasi.
 Nawashukuru wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF
wakiongozwa na Makamu wangu Bwana Michael Wambura,
 Nawashukuru Wadhamini wetu mbalimbali wanaoshirikiana
na TFF kufanikisha shughuli za Mpira wa Miguu,
 Nawashukuru wajumbe wa Kamati mbalimbali za TFF
zilizoundwa na Uongozi wangu,
 Nawashukuru wajumbe wote wa Sekretarieti ya TFF
wakiongozwa na Kaimu Katibu Mkuu Bwana Wilfred Kidao,
 Nawashkuru Waandishi wa Habari wa Vyombo vyote kwa
namna mnavyoendelea kutuunga Mkono kwa kuwa sehemu
ya Shughuli za Mpira wa Miguu kupitia kalamu, mic na
kamera zenu,
 Nawashkuru Viongozi wa Vilabu mbalimbali nchini,
 Nawashukuru wachezaji wote wa Mpira wa miguu nchini
 na mwisho nawashukuru Wadau wote mbalimbali wa Mpira
wa Miguu kwa namna zote tunavyoshirikiana
2 Tanzania Football Federation
web:www.tff.or.tz*youtube:TFFtv*fb:tfftanzania*insta:@tanfootball*twiter:tanfootball
SIKU120
za
Rais KARIA
2.0 UTANGULIZI
Naanza tena kutanguliza kuwatambua Wenyeviti na Marais wote
wa FAT na TFF waliopita kabla yangu wakikiongoza chombo hiki
kwa namna na nyakati tofauti mpaka kufikia name kuendeleza
kuanzia siku nilipoishia. Kuna kazi kubwa mbalimbali zimefanywa
huko nyuma na pia kuna changamoto na mapungufu na hivyo kazi
ya kwanza ya Uongozi wangu na kupembua pumba na mchele na
kuchukua njia sahihi nikiongozwa na DHAMIRA na ILANI ambayo
ndio ahadi mama niliyoiweka kwa Watanzania wote wakiongozwa
na wadau wa Mpira wa Miguu.
Ni vema pia kuwakumbusha “FIRST XI ya KARIA” ambayo
nitahakikisha inatekelezwa ipasavyo na mahitaji yoyote ya
nyongeza na Marekebisho yatazingatiwa kwa weledi:
2.1 “First XI” ya KARIA
1. Nidhamu ya Muundo na Mfumo wa TFF
2. Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Ufukweni
3. Mafunzo na Ujenzi wa Uwezo
4. Mapato na Nidhamu za Fedha
5. Miundombinu na Vifaa
6. Maboresho Bodi ya Ligi
7. Ushirikiano na Wadau
8. Udhamini na Masoko
9. Maboresho ya Mashindano
10. Uimarishaji wa Mifumo ya Kumbukumbu
11. Tiba ya Changamoto za Waamuzi na Uamuzi
2.2 Na nilisisitiza pia Uimara wa Ilani yangu utazingatia Mambo
MANNE ambayo ni:
1. Kupambana na Rushwa, Upendeleo na Uonevu
2. Mpango Mkakati wa TFF (Strategic Plan)
3. Mpango wa Maendeleo ya Vijana (Youth Development Programme)
4. Vipaumbele na Uwajibikaji na Uzalendo
Tanzania Football Federation
web:www.tff.or.tz*youtube:TFFtv*fb:tfftanzania*insta:@tanfootball*twiter:tanfootball 3
SIKU120
za
Rais KARIA
2.3 Napenda pia kuwatambua Wadhamini wote wa TFF
wakiongozwa na Mwenyekiti wao Bwana Steven
MASHISHANGA…..
“na hapa naomba nimzungumzie kidogo Mdhamini wetu
Bwana Joel Nkaaya BENDERA, Kocha wetu aliyeiletea sifa
kubwa Tanzania, Mkufunzi wa Makocha nchini aliyekuwa na
Daraja la Juu, Kiongozi aliyeshiriki katika Nyanja nyingi za
Uongozi wa Michezo na Serikali mpaka kustaafu kwake na
hatimaye kutangulia mbele ya haki, na naomba sasa sote
tusimame kwa dakika moja kwa heshima ya kumbukumbu
yake”
3.0 TATHMINI
Katika Utangulizi huu Naomba kuwajulisha kuwa mara baada ya
kuchaguliwa Kazi yangu ya Kwanza na Kamati yangu ya Utendaji
ilikuwa kuendelea kushughulikia kiutendaji mambo yaliyokuwa
yakiendelea na kazi ya pili ikiwa ni kuanza Tathimini ya hali halisi
ya TFF tulivyoikuta.
Katika Uchambuzi wa Tathmini za kipindi kifupi tulibaini mambo
kadhaa ambayo yalitusaidia kuona namna bora ya kuyaendea
mambo kwa mazingatio ya Ilani yangu ya Uchaguzi na Miongoni
mwa Matokeo ya Tafiti hiyo ilikuwa kubaini vitu viwili vikubwa
ambavyo ni HALI HALISI YA TAASISI na CHANGAMOTO
ambavyo navyo vilizaa muonekano wa FURSA kadhaa. Masuala
ya Utendaji wa shughuli za kila siku tulizozikuta zilifanyiwa kazi
ipasavyo kwa muda mfupi na Kaimu Katibu Mkuu Bwana Salum
Madadi kabla ya kumkabidhi Kaimu Katibu Mkuu Bwana Wilfred
KIDAO ambaye anaendelea na majukumu hayo mpaka sasa.
4 Tanzania Football Federation
web:www.tff.or.tz*youtube:TFFtv*fb:tfftanzania*insta:@tanfootball*twiter:tanfootball
SIKU120
za
Rais KARIA
3.1 Hali Halisi
Miongoni mwa Mambo yaliyobainika kama HALI HALISI baadhi
yake ni pamoja na:
 Kukosekana Mpango Mkakati wa Taasisi
 Uimara na Utendaji hafifu wa Sekretariet ya TFF.
 Kutokuwepo Mpango wa Maendeleo ya Vijana
Unaotekelezwa
 Taasisi kutokuwa na fedha za kutosha za kujiendesha
 Kutokuwepo Matumizi sahihi ya Vyombo vya TFF
 Kutokuwepo Kalenda thabiti ya Matukio ya TFF
 Kukosekana Ratiba na Taratibu thabiti za Vikao.
 Matumizi yasiyo sahihi ya Kamati ya Utendaji na Kamati
ndogo.
 Mahusiano yasiyoridhisha ya TFF na Chombo chake cha
TPLB
 Mahitaji ya Maboresho kwenye Mashindano na Kanuni zake
 Kutokuwepo muelekeo wa kuifanya TPLB kuwa chombo huru.
 Taasisi kukosa Idara ya Ukaguzi wa ndani
 Kutokuwepo Mipango madhubuti kwenye Uwekezaji
Miundombinu
 Kutokuwepo Mpango au muelekeo wa Uhamasishaji
Udhamini kwa TFF, Vilabu na wanachama wa TFF.
 Malalamiko mbalimbali kutoka kwa wadhamini
 Nidhamu na Utaratibu Mbovu wa Matumizi ya Fedha
 Kushindikana kufanyika Mkutano Mkuu wa TFF.
 Kukosekana Mpango wa Ushiriki wa Timu zetu Kimataifa
 Malalamiko na Mapungufu mengi kwenye Mashindano
Mbalimbali.
 Kukosekana Mfumo wowowte wa Utafiti kukidhi Mipango ya
Maendeleo na Utatuzi wa Changamoto hasa
zinazozungumiziwa sana.
Tanzania Football Federation
web:www.tff.or.tz*youtube:TFFtv*fb:tfftanzania*insta:@tanfootball*twiter:tanfootball 5
SIKU120
za
Rais KARIA
3.2 Changamoto
Miongoni mwa Baadhi ya Changamoto ambazo nyingine zinaendelea
kufanyiwa upembuzi ni pamoja na:
 Kukosekana kwa Udhamini wa kutosha kwenye Uendeshaji wa Vilabu,
Vyama, Mashidano na Matukio ya Mpira nchini.
 Dhana ya Rushwa katika Mpira wa Miguu.
 Kukosekana Weledi wa kutosha na Viongozi sahihi na upungufu wa
nyongeza za uwezo wao katika Uendeshaji wa Shughuli za Mpira nchini.
 Kukosekana kwa Mfumo thabiti wa Utambuzi wa Vipaji na Uendelezaji wake
ikiambatana na mifumo ya kumbukumbu zinazohusiana nazo.
 Kukosekana kwa Vituo Madhubuti vya kutosha vya uibuaji wa vipaji na
mafunzo ya mpira wa miguu kwa watoto na vijana nchini.
 Uimara usiokidhi wa kiwango cha Mashindano ya Mashule nchini na
changamoto za muunganiko wake na Mfumo wa Maendeleo ya Vijana na wa
Mpira nchini.
 Vilabu vingi kukosa Mifumo Imara ya kiMuundo, kiUongozi na kiUendeshaji
na mapungufu ya utii wa Mifumo iliyopo.
 Mitazamo hasi kutoka kwa baadhi ya wadau wa Mpira wa Miguu na
WanaHabari na Ukosoaji unaolenga Kuzorotesha na kuharibu taswira nzima
ya Mpira wa Miguu nchini.
 Kukosekana Muunganiko sahihi wa Matumizi ya rasilimali Serikali kwa
Maendeleo na Uendeshaji wa Mpira wa Miguu nchini.
 Uchakavu na Ukosefu wa Viwanja vya Mpira wa Miguu nchini vilivyo katika
viwango bora/sahihi vya kufundishia na kuchezea.
 Upungufu wa Makocha wenye weledi na Ujuzi wa kutosha kwenye Maeneo
ya Utambuzi, Uendelezaji na Uendeshaji wa mafunzo nchini.
 Dhana ya kutoaminiana na uwepo wa Uzalendo pungufu na Umoja katika
eneo kubwa la Uendeshaji wa Mpira nchini.
 Dhana ya Rushwa, Upendeleo na Dhuluma kwenye Uendeshaji wa
Mashindano na Uongozi wa Mpira wa Miguu nchini.
 Upungufu mkubwa wa Maadili miongoni mwa Wachezaji, Viongozi, Waamuzi,
Waandishi wa Habari na wadau wengine katika shughuli za Mpira nchini.
 Udhaifu katika utii wa Mifumo ya Upatikanaji Viongozi katika maeneo
mbalimbali ya Uongozi wa Mpira wa Miguu nchini.
 Mapungufu ya Ithibati ya DHAMIRA kwenye eneo kubwa la Utekelezaji wa
shughuli za Mpira wa Miguu nchini.
 Changamoto Nyingi za Kiuendeshaji na uwajibikaji zinazoikabili TPLB
 Changamoto ya Uelewa wa Kutosha kwa Baadhi ya Viongozi wa Mpira
 Mfumo wa kiElektroniki wa Uingiaji Viwanjani na kukosekana unaofaa zaidi
 Kupungua sana kwa Washabiki Viwanjani
 Uwepo wa Kilabu nyingi katika eneo dogo na Kilabu nyingi kukosa uwezo wa
Kujiendesha
 Kushindwa kwa Wanafamilia ya Mpira wa Miguu Kutambua Athari
Zinazoweza kututokea mbeleni kutokana na Matendo yetu ya leo kama
ambavyo ilishindikana kubaini atahri za yaliyotokea nyuma wakati yanatokea
na ambayo yanatuathiri leo.
 Kutoaminika kwa Viongozi wa Mpira wa Miguu miongoni mwa Wadau wao na
hasa muhimu
 Tishio la HIV-AIDS kwa wachezaji kadri wanavyoimarika kimaendeleo.
6 Tanzania Football Federation
web:www.tff.or.tz*youtube:TFFtv*fb:tfftanzania*insta:@tanfootball*twiter:tanfootball
SIKU120
za
Rais KARIA
3.3 Mipango
Baada ya kubainika kwa kiasi cha wakati husika Hali Halisi na
Changamoto kazi iliyofuata ilikuwa kuimarisha wazo na kuanza
kujenga Mipango ya kukabiliana na Matokeo ya Tafiti na
Changamoto zake. Mipango Mingi kadhaa imeanza
kushughulikiwa tayari kwa kupitishwa kwenye kamati ya Utendaji
ambapo Msingi Mkuu wa kila Mpango ni Tafsiri ya Utekelezaji wa
Mpango Mkakati (Strategic Plan) ambayo imekwishaundwa na
TFF na sasa ikisubiria kuzinduliwa Rasmi. Kwa Msingi wa Uimara
wa Ilani yangu ni wazi katika Mpango Mkakati huu tumeweka
Vipaumbele na Kuijenga Sekretariet katika Sura ya Uwajibikaji
tunaomaanisha na kukusudia. Mpango wa Maendeleo ya Vijana
(youth Development Programme) ni sehemu ya Mpango Mkakati
lakini nimeipa nafasi ya kipekee kwa umuhimu na uzito kwa kuwa
miongoni mwa Matokeo ya Hali Halisi na Changamoto kubwa
zaidi zilizobainishwa ikihusisha Mfumo wetu wa Utambuzi,
Uzalishaji na Uendelezaji wachezaji nchini.
Mipango Mingi inaendelea kujengwa ikijipambanua kwa maeneo
yaliyopewa Vipaumbele na TFF itazindua baadhi yake hadharani
kupitia Matayarisho yatakayofanywa na Mipango mingine itaingia
kwenye UTEKELEZAJI bila ulazima wa kuzinduliwa kwake.
Tunawaomba Watanzania wote kuwa Tayari kuipokea Mipango
Mbalimbali inayotafsiri Utekelezaji wa Mpango Mkakati
unaozingatia ILANI yangu na ninyi kama Wahariri kwa dhati kabisa
tunawaomba mtoe Vipaumbele kwa Msingi wa Uzalendo
kuhakikisha tutatatua kwa pamoja Matatizo ya Mpira wetu. TFF pia
inaamini kwenye kupokea Maoni na Ushauri zaidi katika mipango
hiyo na mingine yetu itakayowajia na hata nje ya Mipango hiyo
kutupa nafasi ya kufanya Maboresho na Marekebisho muhimu
yenye TIJA.
Tanzania Football Federation
web:www.tff.or.tz*youtube:TFFtv*fb:tfftanzania*insta:@tanfootball*twiter:tanfootball 7
SIKU120
za
Rais KARIA
Miongoni mwa Mipango iliyopewa kipaumbele kwa sasa katika
kutafsiri Utekelezaji wa Mpango Mkakati unaozingatia ILANI ya
Rais Karia ni pamoja na:
1. Mpango wa Jumla wa Utekelezaji wa TFF Strategic Plan
2. Mpango wa Maendeleo wa Taifa Stars
3. Mpango wa Mabadiliko na Maboresho TPLB
4. Mpango wa Uhamasishaji na Ufanikishaji Udhamini
5. Mpango wa Ushirikiano Serikali na Mashirikisho ya Kimataifa
6. Mpango Maalum wa Waamuzi na Uamuzi
7. Mpango wa Weledi kwa Wchezaji (HIV – AIDS na MADAWA HARAMU)
8. Mpango wa Ukamilishaji wa Sekretariet na Ufanisi.
9. Mpango wa Uwekezaji Miundombinu ya TFF
10. Mpango wa Mapambano Dhidi ya RUSHWA
11. Mpango wa Mashirikiano ya Maboresho ya Viwanja vya wadau
12. Mpango wa Maandalizi U17 AFCON – Tanzania 2019
13. Mpango wa Utekelezaji kwa Leseni za Vilabu
14. Mpango Mkakati wa Hamasa ya Mtazamo Chanya (PlayFair & Be+)
15. Mpango wa Mapambano Dhidi ya HIV-AIDS na Madawa Haramu
16. Mpango wa Maendeleo ya Vijana (Youth Dev Programme)
3.4 Misingi na Imani ya TFF
TFF inatambua uzito na wingi kwa idadi wa Mipango iliyopewa
Kipaumbele na inatambua wajibu ulio mbele yake wa Utekelezaji
na kadhalika TFF inatambua Mahitajio ya wadau wengine katika
Ufanikishaji, aidha mahitaji ya Uwezeshaji Mkubwa lakini kubwa
zaidi pamoja na uzito wa yote hayo ni KUUNGWA MKONO na
jamii ya Watanzania kwa kutanguliza Uzalendo kwa nchi yao,
Kushiriki ipasavyo kwenye Mpngo wa Mtazamo Chanya na tuimbe
kwa Pamoja kauli mbiu ya PLAYFair&Be+ (Sote tuwe waungwana
katika mchezo wetu pendwa na siku zote tubaki tukiamini kwenye
kufanikiwa na kuaminiana huku kila mmoja akiitumia nafasi yake
vema kufanikisha na kujenga na si kubomoa)
8 Tanzania Football Federation
web:www.tff.or.tz*youtube:TFFtv*fb:tfftanzania*insta:@tanfootball*twiter:tanfootball
SIKU120
za
Rais KARIA
TFF inaamini kwenye kukosea kwa binaadamu yoyote na tunatoa
ahadi ya kukosea kama binaadamu na si kukosea kwa hila,
ubinafsi au kujinufaisha mmoja mmoja na vivyo hivyo tunaiomba
jamii ya wanahabari na wadau wote kuwa na Mtazamo chanya
zaidi, kukosoa kwa kujenga na si kuubomoa mpira wetu, kutoa
maoni kadri iweekanvyo kwa nia njema kwa DHAMIRA dhahiri
kutok moyoni mwako. TFF itatengeneza mfumo rasmi wa
uwasilishaji kwa urahisi maoni na mawazo ya wadau wetu. TFF
inaamini njia hii itausaidia Mpira kusaidiwa zaidi ya ilivyo sasa
kwani kazi iliyo mbele ya TFF ya kurekebisha na kufanikisha ni
kubwa na inahitaji ushiriki wa kila mmoja na kila sekta husika na
kuingiza sekta nyinginezo kwa umoja na nguvu ya umoja wetu
wanafamilia ya Mpira wa miguu.
TFF inakuja mbele ya jamii leo hii kuwasilisha Taarifa hii na
kuonyesha DIRA na MUELEKEO wa Mpira wa Miguu nchini baada
ya siku 120 zilizofanyiwa kazi hii zilizoanzia tarehe 12 agosti
mpaka tarehe 09 disemba 2017. Katika kipindi hicho TFF
imeendelea kushughulika na Utekelezaji wa Majukumu yake ya
kila siku mengi yakizingatia ILANI ya Rais ambapo mambo kadhaa
kutoka ILANI yangu yameendelea kufanyiwa kazi kwa Mafanikio
na kuleta sura tofauti na ya matumaini makubwa ya Uendeshaji wa
Mpira wa Miguu nchini. Msingi Mkuu wa mabadiliko haya zaidi ya
kila Mpango na ILANI ni DHAMIRA ya dhahiri inayoonyeshwa
nami binafsi kama Rais na Mkuu wa Taasisi na Msimamizi Mkuu
wa Sekretariet inayoongozwa na kijana Mchapa Kazi Wilfred
KIDAO ambaye anazitafsiri ipasavyo sifa za CV yake kama kijana,
mchezaji wa zamani wa kiwango cha juu nchini, msomi na
kiongozi aliyepitia ngazi tofauti za Uongozi wa Mpira wa Miguu
akitafsiri kwa vitendo kwa Utendaji wake ambapo Mpaka sasa
hajaniangusha na nina matumaini makubwa nae.
Tanzania Football Federation
web:www.tff.or.tz*youtube:TFFtv*fb:tfftanzania*insta:@tanfootball*twiter:tanfootball 9
SIKU120
za
Rais KARIA
4.0 UTEKELEZAJI
Uongoziwangu Umefanya mambo mengi ya Kiilani na kiutendaji
wa kawaida ambapo Miongoni mwa baadhi ya mambo ambayo
yamefanyiwa kazi ipasavyo katika siku 120 za kwanza za Uongozi
wangu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ILANI yangu ni angalau
50 tu ni kama inavyoainishwa:
1 Tathmini ya Hali ya Shirikisho
2 Utambuzi na Uanishaji wa Changamoto
3 Utambuzi, Uhakiki na Uratibu wa Fursa
4 Ujenzi wa Mpango Mkakati wa TFF (Strategic Plan)
5 Ujenzi wa Mpango wa Utekelezaji wa Mpango Mkakati
6 Ujenzi wa Mipango Mbalimbali ya Maendeleo na Uendeshaji
7 Kuimarisha Mahusiano na Serikali na Mashirikisho
8 Uimarishaji wa Utawala Bora na Matumizi ya Vyombo vya TFF
9 Mafanikio ya mabadiliko ya Mfumo wa Fedha na Malipo
10 Kasi na Uboreshaji wa Masuala ya Kawaida ya Kiuendeshaji
11 Uimarishaji na Utekelezaji wa Maandalizi ya u17 AFCON 2019
12 Kuimarishwa na kuboreshwa kwa Ligi Kuu ya Wanawake
13 Kuimarishwa na Kuboreshwa kwa Kombe la Shirikisho
14 Utii wa Katiba na taratibu kwa Ofisi ya Rais wa TFF
15 Uhuru wa Kufanya Kazi kwa Sekretariet
16 Ujenzi wa Sekretariet na Maboresho ya Mahusiano kikazi
17 Matumizi sahihi na mazingatio kwa vyombo na kamati za TFF
18 Kurejesha na Kuimarisha Heshima ya Ofisi za TFF
19 Kuundwa kwa Kamati mbalimbali kuisaidia Kamati ya Utendaji
20 Kuhuishwa kwa Utekelezaji wa suala la Leseni za Kilabu
21 Kuimarishwa kwa Programu za Timu za Taifa za Vijana
22 Ugawaji wa Mipira na Vifaa vya Mafunzo kwa Vijana Mikoa yote
23 Maboresho ya Mfumo wa Ligi Kuu ya Vijana (u20PL)
24 Matayarisho ya Timu ya Taifa ya u17 AFCON 2019
10 Tanzania Football Federation
web:www.tff.or.tz*youtube:TFFtv*fb:tfftanzania*insta:@tanfootball*twiter:tanfootball
SIKU120
za
Rais KARIA
25 Kufanyika kwa kozi 20 tofauti katika mikoa ndani ya siku 120
26 Viongozi na Maafisa kushirika Mafunzo na ziara Kimataifa
27 Kupatikana Udhamini wa KCB Bank
28 Kushughulikia Matatizo ya Masharti ya Misaada ya FIFA
29 Kuimarika Mahusiano na Ulipaji Kodi TRA na Mifuko ya Jamii
30 Kuanzishwa Ukaguzi wa Ndani kwa Sekretariet ya TFF
31 Maboresho ya Kanuni za Fedha za TFF na usimamizi wake
32 Maboresho ya Mfumo wa Manununzi
33 Maandalizi ya Mpango wa Uwekezaji Karume na Tanga
34 Kuanza Mazungumzo na Wamiliki wa Viwanja kwa Maboresho
35 Ukarabati na Mazingira ya Ofisi za TFF
36 Ujenzi wa Uwanja wa Soka la Ufukweni Coco Beach
37 Kuanza kwa Tathmini ya Mabadiliko TPLB na Uhuru zaidi
38 Watanzania kadhaa kuteuliwa Kamati za CAF na CECAFA
39 Kuimarika kwa Utendaji na Mahusiano na Wadhamini wetu
40 Kupatikana Uongozi TPLB
41 Kuanzishwa na kuchezwa Ligi Ndogo ya Wanawake
42 Maboresho ya Utoaji Tuzo za Ligi Kuu
43 Kuchezwa Soka la Ufukweni na Mipango ya kucheza kimataifa
44 Taifa Stars kuendelea kushiriki Kimataifa kwa Mafanikio
45 Kilimanjaro Stars kushiriki Kombe la Chalenji Kenya
46 Matayarisho ya Mifumo Mipya ya Usajili, Utunzaji Kumbukumbu
47 Rais wa TFF kushughulikia suala la Matatizo ya Uamuzi nchini
48 Kufanya Vikao na Vialbu wawakilishi wan chi Kimataifa
49 Kushiriki Utatuzi wa Matatizo ya Vilabu mblimbali
50 Uanzishwaji mara moja wa Utekelezaji wa Ilani ya Rais Karia
Tanzania Football Federation
web:www.tff.or.tz*youtube:TFFtv*fb:tfftanzania*insta:@tanfootball*twiter:tanfootball 11
SIKU120
za
Rais KARIA
4.1 TATHMINI YA UTEKELEZAJI wa ILANI
Uongozi wangu tumefanya utekelezaji wa majukumu
yaliyoainishwa katika “First XI” (Ilani) yangu kama
ilivyochambuliwa kwa kiasi hicho kilichowezekana. Ifuatayo ni
Tathmini ya utekelezaji wa Dondoo (Vipengele vya Ahadi) za Ilani
(AHADI ZANGU) zikitafsiri Utekelezaji wa Ilani yenyewe kama
Ifuatavyo:
First XI
ILANI
Dondoo
Zilizoainishwa
Dondoo
Zilizoshughulikiwa
Dondoo
Bado
Wastani kwa
Asilimia
I 5 5 0 100%
II 8 4 4 50%
III 6 5 1 83%
IV 11 7 4 64%
V 5 3 2 60%
VI 4 4 0 100%
VII 4 2 2 50%
VIII 7 7 0 100%
IX 7 5 2 72%
X 2 2 0 100%
XI 6 2 4 33%
65 46 19 71%
Tathimini hii imejielekeza kwa kushughulikiwa kwa Masuala
niliyoainisha kama AHADI zangu kwa Wanafamilia na Wajumbe wa
Mkutano Mkuu. Katika hayo tumeweza kufanyia Kazi asilimia 71% za
Masuala yote ndani ya kipindi cha siku 120 za kwanza za Uongozi
wangu pamoja na Changamoto zote zinazoikabili TFF.
Haya ni Mafanikio ya kwanza kwa Kamati ya Utendaji ninayoiongoza
kwamba ndani ya kipindi cha siku 120 kuweza kutekeleza na
kushughulikia Kila ILANI kwa utofauti wa asilimia tu na hivyo ni Ishara
kwamba TFF sasa inatengeneza uelekeo kuelekea kukidhi haja na
shauku ya WaTanzania katika Mafanikio ya Mpira wa Miguu.
Sehemu kubwa ya Mambo ambayo hayajashughulikiwa Ipasavyo
yanasomeka kwenye Mipango ya TFF iliyoainishwa kwenye Taarifa hii
ikiwa imejielekeza kwenye Utekelezaji wa Ahadi zangu, Shughuli za
Kawaida za TFF na Utatuzi wa Changamoto baada ya Tathmini ya
Taasisi. Mipango iliyoainishwa humu inawezekana tu kwa TFF kupata
Ushirikiano kwa wadau muhimu na TFF kwa ujumla wake haina shaka
na Imani hiyo. Dhamira ni Njema, Utendaji wa Kiwango, Uaminifu,
Uadilifu na Nidhamu, Uwajibikaji na Utatuzi ni dhahiri DHAMIRA yangu
na Uongozi wangu kufanya Mabadiliko Makubwa kwa matarajio ya
Matokeo Makubwa zaidi haina shaka.
12 Tanzania Football Federation
web:www.tff.or.tz*youtube:TFFtv*fb:tfftanzania*insta:@tanfootball*twiter:tanfootball
SIKU120
za
Rais KARIA
5.0 UZINDUZI WA MPANGO MKAKATI (Strategic Plan)
Mpango Mkakati wa TFF ni Nyaraka muhimu sana iliyo na
Muelekeo na Mpango Mkuu wa Utekelezaji Shughuli za TFF katika
kipindi husika. TFF imejipangia Programu nyingi kadhaa ambazo
zitautafsiri Mpango huu Mkuu kwa Uchambuzi na Mazingatio ya
Vipaumbele vilivyowekwa na Programu na Mipango chambuzi
itatolewa Baada ya Uzinduzi rasmi wa Mpango Mkakati wa TFF (tff
strategic plan) na Mpango wa Utekelezaji wake (Action Plan).
Mchakato unalazimisha mahitaji ya Ujenzi na Uchakataji wa
Mipango ya Utekelezaji na maendeleo ambayo inaendelea
kujengwa tayari kwa kuthibitishwa na Kamati ya Utendaji katika
kikao chake cha JANUARI 2018 ili kuwa tayari kwa matumizi na
utendaji. Pamoja na Ujenzi huo wa Mipango bado TFF inaendelea
kushughulikia maeneo miongoni mwa Mipango hiyo na shughuli
nyingine za TFF kwa mazingatio ya wakati na msingi wa jambo na
mpango husika.
TFF inatangaza Rasmi na kuwaomba kushiriki Katika Uzinduzi wa
MPANGO MKAKATI wake utakaofanyika tarehe XX/01/2018
katika Utaratibu tutakaotangaziwa.
6.0 FURSA
TFF katika tathimini zake ndani ya siku 120 za kwanza za Uongozi
wangu TFF imetathimini pia FURSA mbalimbali ambazo zinaweza
kuharakisha na kusaidia Maendeleo ya Mpira wa Miguu nchini na
imeziona baadhi ya Changamoto kama sehemu ya Fursa kwa
kuzibadili kimtizamo na kuzifanyia kazi. Aidha TFF imebaini baadhi
ya Fursa nyingine ambazo hazitumika ipasavyo kwenye Mpira wa
Miguu na namna bora ya kuyafanyia kazi mambo mangine kadhaa
kwa namna tofauti ambayo nayo pia ni fursa pana kwa faida ya
Mpira wa Miguu nchini.
Fursa hizi kwa msingi wake na uzito wa kuwa sehemu ya Mkakati
wa Utekelezaji Mpango Mkakati wa TFF na Programu zake
inazoshughulikia kwa sasa zinaendelea kupangiliwa vema ili
kusifanyike makosa na kuhakikisha zinafanikiwa na kufanikisha
kwa asilimia kubwa kama sio zote
Tanzania Football Federation
web:www.tff.or.tz*youtube:TFFtv*fb:tfftanzania*insta:@tanfootball*twiter:tanfootball 13
SIKU120
za
Rais KARIA
7.0 MAJUMUISHO
Mipango na Programu hizi za TFF zinajielekeza kuanza
Utekelezaji wake 2018 na ni dhahiri unaweza kuona kwa dhati
uzito wa majukumu yaliyo mbele ya Uongozi wangu. Katika
utekelezaji mambo kadhaa muhimu ni vema yakaeleweka kwa
ufafanuzi kama ifuatavyo:
7.1 Kila Mpango utakaotolewa na kuwekewa Utaratibu wake na
Kuwekwa hadharani utaainisha Namna ya utekelezaji wake
ipasavyo, Muda na Matarajio ya MATOKEO MAKUBWA zaidi
kwa eneo husika na mahusiano na mafanikio ya Ujumla wake
kwa TFF.
7.2 Ujenzi wa Mipango na Programu hizi ni wazi na lazima
kushirikishe Wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya TFF na
pengine Nje ya Tanzania na baadhi ya ukamilishaji wa
Mipango na mwanzo wa Utekelezaji unaweza kutegemea
mamlaka nyingine na hivyo uwezekano ni mkubwa wa uwepo
wa Changamoto na TFF kwa kuwa inatabiri baadhi ya
Changamoto kadhalika inajipanga namna ya kukabiliana
nazo.
7.3 Mipango yote iliyoainishwa inategemea Uwekezaji na
Uwezeshaji katika maeneo ya Rasilimali watu, Rasilimali
Fedha, Rasilimali Muda na Rasilimali Mamlaka na hivyo TFF
inaendelea kupambana na mazingira yote hayo kwa kuamini
na kuhusisha Muingiliano madhubuti kwa baadhi ya Mipango
na Programu kwa kuamini na kutambua kuwa ukamilifu na
utekelezaji wa baadhi yake zitategemea pia Mafanikio ya
Mipango na Programu nyingine
7.4 TFF inaomba Ushirikiano, Uvumilivu, Kuungwa Mkono,
kusaidiwa kwa namna yoyote iwezekanavyo, watu wa
kujitolea watakaoombwa, na Uimarishwaji wa DHANA ya
PlayFair&BE+ ili kurejesha na kuendelea kujenga Thamani ya
Mpira wa Miguu nchini na kuleta Mafanikio tarajiwa.
14 Tanzania Football Federation
web:www.tff.or.tz*youtube:TFFtv*fb:tfftanzania*insta:@tanfootball*twiter:tanfootball
SIKU120
za
Rais KARIA
8.0 UZALENDO KWANZA, Tanzania ndio KWETU na huu ndio
Mpira wetu, jukumu ni letu sote, tunaongoza Mapambano
asipatikane anayerudi Nyuma ama kutusaliti au kutukwamisha.
Tupeane SHIME na lazima tufike kwa pamoja na UMOJA WETU.
MWISHO:
TFF kwa Taarifa hii inakaribisha Maoni na Maboresho yoyote kutoka
kwa wadau wake na tunawaahidi usikivu wa hali ya juu na tunaomba
Imani ya kila Mdau kwa Uongozi wangu na kuungwa Mkono kwa
Maendeleo ya Mpira wetu ambamo wadau wote hatuna namna ya
kujitoa. TFF kwa sasa itaendelea kutumia anuani zake zilizozoeleka
kupokea taarifa, maoni na mitazamo kutoka kwa wadau na
itatengeneza Utaratibu rafiki zaidi na bora ikihitajika wa kuweza
kuwafanya wadau kuwasilisha maoni yao kirahisi zaidi.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanznania
Tanzania Football Federation
♯PLAYFair & Be+
(shiriki kiungwana kwa haki na dhati na kuwa na mtazamo chanya siku zote)
_____________
Wallace KARIA
Rais
TFF
Mawasiliano:
Katibu Mkuu (Kaimu)
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
Uwanja wa Karume
Mtaa Uhuru/Shaurimoyo
ILALA
P O Box 1574, Dar es Salaam
TeleFax +255 22 286 1815
Email: tanfootball@tff.or.tz
Twiter: @tanfootball
Insta: @tanfootball
Facebook: tfftz
Youtube: TFFtv
Web: www.tff.or.tz
Tanzania Football Federation
web:www.tff.or.tz*youtube:TFFtv*fb:tfftanzania*insta:@tanfootball*twiter:tanfootball 15
SIKU120
za
Rais KARIA

Be the first to comment

Leave a Reply