Robo fainali AFCON timu nane zafahamika

Mzunguko wa hatua ya robo fainali ya AFCON 2017 umethibitishwa baada ya Misri kujipatia tiketi yake ya ushiriki siku ya Jumatano.

Waliwachabanga Black Stars wa huko Ghana kwa bao 1-0 na kumaliza wakiwa kileleni mwa Kundi C na wanajiandaa na hatua ya robo fainali inayowakutanisha miamba tupu wa Afrika ya Kaskazini dhidi ya Morocco.

Siku ya Jumamosi, Burkina Faso wanakutana na Tunisia na Senegal wanakwaana na Cameroon kwenye robo fainali nyingine. Misri hawajaruhusu goli lolote kwenye AFCON 2017. Kwa upande mwingine, Ghana, wao wataumana na DR Congo kwenye robo fainali kwa sababu walipita ingawa walipokea kichapo.