Rose Barkley anakaribia kujiunga na Chelsea

Swali kubwa ni kwamba wapi kiungo huyo mchezaji atafitishwa kuendana na mifumo ya uchezaji ya meneja wa Chelsea Antonio Conte?

Chelsea inakaribia kukamilisha dili la kumchukua kiungo Rose Barkley wa Everton kwa ada ya paundi milioni 15 baada ya mpango huo kujaribiwa wakati wa kiangazi kabla ya baadaye kushindikana.

‘Nadhani ni fursa nzuri kwa klabu kumnunua mchezaji huyu’ amesema Antonio Conte .

Tunamzungumzia mchezaji wa kingereza, kijana. Ana kila sifa ya kuichezea Chelsea. Nadhani klabu imeamua kwa uwekezaji huu na mkataba wake.

Be the first to comment

Leave a Reply