Saidi Ndemla afuzu majaribio katika klabu ya Eskilstuna ya Sweden

Saidi Ndemla amefanikiwa majaribio yake nchini Sweden.

Mchezaji Said Hamis Juma (Ndemla) amefanikiwa kufuzu kwenye majaribio yake ya kucheza Soka la kulipwa barani Ulaya.

Ndemla aliyekuwa nchini Sweden kwa majaribio kwenye klabu ya Eskilstuna ya huko.anatarajiwa kurejea nchini siku ya jumatatu inayokuja.

Taarifa ya Mkuu wa idara ya Habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Haji Manara kwa wanahabari iliyotolewa hii leo imesema mara baada ya kurejea kwa kiungo huyo klabu za Simba na Eskilstuna zitaanza mazungumzo ya kimkataba ili kumwezesha kiungo huyo kwenda Sweden kwa ajili ya kucheza Soka huko.

Imenukuliwa katika taarifa hiyo ikisema “Kiufupi klabu imefurahishwa na azma ya Ndemla ya kutaka kusonga mbele zaidi, na kama ilivyo desturi na utamaduni wa Simba, klabu haitasita kumruhusu mchezaji yoyote anayepata fursa adhimu kama hiyo itakayomsaidia mchezaji binafsi.klabu na Taifa kwa ujumla”.

Be the first to comment

Leave a Reply