Salah ashinda tunzo ya mchezaji bora wa mwezi Novemba

Mohamed Salah ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Premier League mwezi Novemba

Mohamed Salah ametangazwa mchezaji bora wa mwezi Novemba tuzo inayotolewa na EA SPORTS.

Mshambuliaji huyo wa Liverpool aliyesajiwa kiangazi anakuwa mchezaji wa kwanza kutoka Misri kushinda tuzo hiyo kufuatia kufunga goli saba katika michezo 4 ya timu yake ndani ya mwezi huo.

Alifunga magoli mawili katika mchezo dhidi ya West Ham United, Southampton na Stoke City na goli lingine katika mchezo wa sare dhidi ya Chelsea Chelsea.

Salah ambaye kwasasa anaongoza kwa ufungaji wa magoli katika ligi hiyo inayoendelea kwa kuwa na magoli 13, ameshinda tuzo hiyo inayotokana na kura za wataalamu, manahodha wa vilabu vya ligi kuu na mashabiki wa ligi hiyo akiwashinda wachezaji wingine sita walioteuliwa.

Amewashinda Robbie Brady wa Burnley, Kevin De Bruyne na Raheem Sterling wa Manchester City, Ashley Young wa Manchester United, Eden Hazard wa Chelsea na mlinzi wa Arsenal Shkodran Mustafi.

Be the first to comment

Leave a Reply