Silva aboresha mkataba wake City

David Silva sasa kulipwa paundi 150,000 mkataba wake hadi mwisho wa msimu ujao

Inaarifiwa ya kwamba DAVID SILVA anaelekea kusaini mkataba wa mwingine wa kurefusha uwepo wake ndani ya viunga vya Etihad kwa mwaka mmoja mwingine.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31, amekuwa katika mazungumzo tangu kuanza kwa msimu huku pande mbili hizo zikisuguana kupata muafaka wa masharti ya mkataba wenyewe.

Taarifa zinaeleza kuwa tayari kuna maelewano yamefikiwa na Silva anakaribia kuingia kandarasi nyingine itakayokuwa na malipo ya paundi £150,000 kwa wiki mkataba ambao utamuweka Manchester City hado mwisho wa msimu wa 2019-20.

Be the first to comment

Leave a Reply