Yanga kuanzia nyumbani klabu bingwa Afrika, Simba ugenini Djibouti kombe la Shirikisho

Simba na Yanga kuanzia nyumbani mashindano ya vilabu Afrika

Shirikisho la soka barani Afrika limetoa ratiba ya mashindano ya vilabu barani humo ambapo katika klabu bingwa, Yanga ya Tanzania imepangwa kucheza na St. Louis ya Shelisheli katika raundi ya awali ya mashindano hayo Yanga akianzia nyumbani. Mshindi wa mchezo huo atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Township Rollers ya Botswana na El Merrikh ya Sudani.

Katika kombe la Shirikisho wekundu wa Msimbazi Simba ya Tanzania imepangwa kuanza na Gendarmerie Tnale ya Djibouti na Simba itaanzia ugenini Djiuboti, ambapo mshindi wa mchezo huo atakutana na mshindi kati ya El Masry ya Misri na Green Bualoes ya Zambia.

Droo ya raundi za awali za mashindano yote ya vilabu 2018 imefanyika leo Disemba 13 2017, katika mkutano wa kamati ya mashindano ya vilabu uliofanyika makao makuu ya CAF Cairo, Misri.

Jumla ya timu 59 zitashiriki mashindano ya klabu bingwa 2018 na timu nyingine 54 zitashiriki katika mashindano ya kombe la shirikisho.

Matiafa 8 hayatashirikisha vilabu vyao ambayo Cape Verde, Chad, Eritrea, Namibia, Reunion, Sao Tome & Principe, Sierra Leone na Somalia.

Be the first to comment

Leave a Reply