Thierry Henry akata tamaa na Top 4, Sadio Mane nje hadi mwisho wa msimu

Nyota na nahodha wa zamani wa Thierry Henry amesema hadhani kama timu yake hiyo ya zamani itaweza kumaliza katika moja ya nafasi 4 za juu msimu huu.
The Gunners walikuwa bado wako ndani ya eneo hilo hadi mwezi uliopita lakini vichapo mfululizo kutoka kwa Liverpool na West Brom na kufuatiwa na sare ya 2-2 dhidi ya Manchester City kumeifnaya timu hiyo kudondoka hadi nafasi ya 5 katika msimamo wa ligi.
Licha ya kuwa nyuma kwa alama 4 toka anayeshika nafasi ya ambayo ni Manchester City na Aesenal ikiwa bado na mchezo mmoja mkononi, Henry anaamini Arsenal inawakati mgumu wa kuweza kufuta mwanya huo wa alama na kurejea tena katika nafasi nne za juu.

Bosi wa Liverpool Jurgen Klopp amethibitisha kuwa Sadio Mane atakosa michezo yote iliyosalia msimu huu ambapo kuna michezo 7 ya ligi ya Premier kufuatia kupata maumivu ya mguu.
Winger huyo mwenye umri wa miaka 24 na raia wa Senegal alipatwa na maumivu ya mguu katika mchezo wa ushindi wa bao 3-1 dhidi y Everton wikiendi iliyopita.
Taarifa za awali ziliarifu kuwa majeraha ya Mane yalikuwa madogo, lakini meneja Klopp mapema hii leo amethibitisha kuwa mchezaji wake atahitajika kufanyiwa upasuaji.
Klopp amethibitisha hilo katika kikao cha maandalizi ya mchezo dhidi Stoke City hapo kesho.

Na mshambuliaji wa Hull City Oumar Niasse anaamini kuwa kufanya kazi pamoja na kujituma ndio siri ya kikosi cha Hull kupanda juu kutoka katika ukanda wa kushuka daraja.
Kwa muda mrefu Hull City imekuwa ikigaragara katika ukanda huo, lakini sasa imeanza kupata muelekeo sahihi baada ya kupata ushindi katika michezo mitatu kati ya 4 ya hivi karibuni.
Niasse raia wa Senegal alifunga goli zuri katika mchezo wa ushindi wa bao 4-2 dhidi ya Middlesbrough na amedokeza kuwa siri kubwa ya mafanikio ya kikosi chao ni umoja na kujituma.
“kusalia katika ligi tunajua kunahitaji umoja na kupambana kama kitu kimoja” ndivyo alivyosema Niasse na kukaririwa na tovuti rasmi ya klabu yake.