Twende zetu wiki ya 11 ya Premier League

WIKI ya 11 ya ligi kuu ya soka nchini England itakuwa ni moja kati ya wiki za nguvu kabisa katika kampeni ya msimu huu wa 2017-18 campaign, kwani timu nne zinazopigiwa upatu wa kushinda taji la msimu zitakuwa zikikutana katika michezo miwili.
Jumapili timu kiongozi katika jedwali la msimamo hadi kufikia sasa Manchester City itakuwa mwenyeji wa timu inayojiimarisha ya Arsenal katika dimba la Etihad. Mchezo huo utafuatiwa na ule wa Chelsea kuikaribisha Manchester United, pale Stamford Bridge.
City inaongoza kwa tofauti ya alama katika kilele cha msimamo wa ligi hiyo ikifuatiwa na Manchester United huku Arsenal na Chelsea kila upande ukihitaji matoke kuendeleza matumaini ya nafasi ya kushinda ubingwa wa msimu huu.
Mwenendo chanya wa Arsenal umewafanya mashabiki wa ligi hiyo kuanza kuamini kuwa upinzani katika nafasi nne za juu umeamka upya.

STOKE CITY VS LEICESTER CITY
Arena/Stadium: bet365 Stadium

Bosi mpya wa Leicester Claude Puel atakuwa akisaka ushindi wa pili tangu aingie kazini wakati kikosi chake kitakapokuwa safarini kuifuata Stoke.
Leicester maarufu ‘The Foxes’ imeshinda michezo mitatu tangu Craig Shakespeare alipofutwa kazi, ukiwemo ushindi wa 2-0 dhidi ya Everton mchezo ambao meneja huyo mfaransa alikuwa kazini kwa mara ya kwanza.
Kwa upande wa Stoke City kumekuwa na matokeo yasiyoridhisha kwani imepoteza michezo mitano katika michezo saba ya mwisho ya mashindano yote.
Ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Watford katika mchezo wao wa mwisho wikiendi iliyopita umesaidia kuiondosha katika kilinge cha timu tatu za mwisho katika jedwali la msimamo, huku meneja Mark Hughes akiingia katika mchezo huu kwa lengo la kushinda kwa mara kwanza tangu mwezi Septemba.
PETER CROUCH mwenye magoli matatu msimu huu anatarajiwa kuwepo kikosini baada ya kuponya maumivu madogo ya mgongo, wakati ambapo mlinzi Bruno Martins Indi akiendelea kusalia nje na Geoff Cameron akiwa katika uangalizi kabla ya kuthibitishwa kama yuko fiti kwa mchezo huo.
Bado saga la Adrien Silva linaendelea hivyo Leicester itaendelea kumkosa kiungo huyo huku pia Robert Huth na Matty James wakiwa wanauguza majeraha hivyo nao wataukosa mchezo huo.

Huddlesfield vs West Brom
Arena/Stadium: Kirklees Stadium

Huddersfield inaingia katika mchezo huu ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha 3-0 kutoka kwa Liverpool. Wageni hawa wa msimu huu wameshinda mchezo mmoja tu katika michezo nane iliyopita ya ligi hii.
Kwa upande wa West Brom haijashinda michezo nane baada ya kichapo cha uwanja wa nyumbani cha 3-2 kutoka kwa viongozi wa ligi Manchester City. Vijana wa Tony Pulis wametoka sare michezo minne.
Kwa mara ya mwisho timu hizi zilipokutana ilikuwa ni katika dimba la Hawthorns mwaka 2001 mchezo ambao ulitoa matokeo ya 1-1.
Huddersfield imekuwa ikipambana kupata magoli yakutosha kwani hadi kufikia sasa imeshazifumania nyavu mara 4 katika michezo 5 ya uwanja wake wa John Smith.
Imekuwa ni timu yenye idara bora ya ulinzi ikiwa imefungwa goli moja katika mchezo mmoja inapocheza. Rekodi ya West Brom inapokuwa ugenini sio nzuri ikiwa imefungwa magoli matatu katika michezo mitano inapokuwa ugenini. Timu zote zina uhaba wa magoli msimu huuna mchezo unaweza kuwa mgumu.

SOUTHAMNTON VS BURNLEY
Arena/Stadium: St Mary’s Stadium

SOUTHAMPTON itakuwa ikifukuzia matokeo ya kutokufungwa kwa michezo 4 mfululizo wakati Burnley watakapokuwa wakiwafuata mchezo wa mchana katika dimba St Marys.
Southamton imeshinda michezo miwili katika mechi tisa na hapa itakuwa ikisaka ushindi mwingine nyumbani chini meneja Manuel Pellegrino ikiwa imevuna alama 5 katika michezo 3 ya mwisho.
Burnley imekuwa na kandanda safi ugenini mbali na nyumbani Turf Moor msimu huu, kwani tayari imekusanya alama Anfield, Stamford Bridge na Wembley kabla ya kuharibu mwenendo huo dhidi ya Manchester City.
Itaingia katika mchezo huu ikiwa na mshambuliaji tegemeo Chris Wood ambaye aliukosa mchezo dhidi ya Newcastle lakini sasa anarejea katika kikosi cha kwanza kama hatakuwa na maumivu ya paja.
Nahki Wells ametajwa kuwepo katika benchi kwa mara ya kwanza na inawezekana akapata nafasi ya kucheza kwa mara ya kwanza.
Watakatifu watakuwa na Charlie Austin kwa mara nyingine baada ya kuukosa mchezo wa Brighton kufuatia majeraha.
Southampton imeishinda Burnley katika michezo yao yote 4 ya mwisho ya mashindano yote ikiwemo ya michezo miwili ligi ya Premier msimu uliopita.

NEWCASTLE VS BOURNEMOUTH
Arena/Stadium: St James’ Park

Newcastle United itakuwa ikiikabili AFC Bournemouth ambayo ina garagara katika nafasi ya 19 katika jedwali la msimamo wa ligi.
Katika michezo ya hivi karibuni, Bournemouth ilionekana kuimarika kimchezo licha ya kufungwa 1-0 na watetezi wa taji Chelsea na hata Tottenham Hotspur, nayo ilifanikiwa kupata ushindi wa 2-1 ugenini kwa Stoke City.
Hili ni jaribio gumu kwani Newcastle italazimika kupambana kupata matokeo.

SWANSEA VS BRIGHTON
Arena/Stadium: Liberty Stadium

Brighton & Hove Albion itakuwa ikijaribu kulinda mwenendo wao wa kutokupoteza katika michezo 4 ya mwisho wakiwa ugenini dhidi ya Swansea.
Kikosi cha Chris Hughton kimekusanya alama 5 katika michezo 3 ya karibuni na itakuwa ikielekea Wales kuifuata Swansea kwa mara ya kwanza tangu 2009.
Brighton (Seagulls maarufu) ilichomoza na ushindi wa bao 2-1 mwaka 1983 ukiwa ni mchezo wa mwisho timu hizi kukutana katika ligi kuu, lakini pia zote zilishuka daraja msimu huo.
Sasa ni miaka 34 imepita, Albion inashikilia nafasi ya 12 katika msimu wao wa kwanza wa ligi ya Premier, alama 4 mbele ya kikosi cha Paul Clement ambacho kina alama moja juu ya mstari wa kutenganisha wale wanaoshuka daraja (Yaani bottom three)

EVERTON VS WATFORD
Arena/Stadium: Goodison Park

EVERTON watakuwa wenyeji wa Watford katika mchezo ambao utapigwa Jumapili mchana na itakuwa ikisaka ushindi angalau kumaliza kiu ya ushindi baada ya michezo 4 ya hivi karibuni.
Baada ya Ronald Koeman kuondoshwa kazini na nafasi yake kushikiliwa na David Unsworth, Everton itakuwa inahitaji kupata matokeo katika uwanja wa nyumbani.
TROY DEENEY amefungiwa mchezo mmoja baada ya kukubali kuhusika katika vurugu dhidi ya Joe Allen, hivyo basi hilo litakuwa ni pigo wa wageni.
Lakini Everton pamoja na kuwa na orodha ndefu ya wachezaji majeruhi lakini Nikola Vlasic anaweza kurejea baada ya kuponya maumivu ya kifundo cha mguu.
Everton imepoteza mchezo mmoja tu kati ya michezo 8 ya mwisho timu hizo zilipokutana, yaani imeshinda michezo 5 na kwenda sare michezo miwili.

TOTTENHAM VS CRYSTAL PALACE
Arena/Stadium: Wembley Stadium

SPURS itakuwa na matumaini ya kutumia nguvu ya mwendo wa ushindi wa 3-1 dhidi ya Real Madrid katika michuano ya klabu bingwa, kuwabomoa washika mkia wa msimamo wa ligi ya Premier Crystal Palace.
Pamoja na ushindi dhidi ya Madrid, tukirudi katika ligi ya Premier, Spurts itakuwa inaingia katika mchezo huu ikiwa inakumbuka kipigo cha 1-0 kutoka kwa Manchester United.
Palace inakumbuka matokeo ya sare ya 2-2 dhidi ya West Ham ambapo goli la dakika za majeruhi la Wilfried Zaha likiinyima wagonga nyundo matokeo ya kuondoka na alama zote tatu.
Spurs imeshinda michezo yote 4 ya mwisho ya ligi dhidi ya Palace, ikiruhusu kufungwa goli moja, mara ya mwisho kufungwa ilikuwa 2-1 Januari 2015 pale Selhurst Park.

Be the first to comment

Leave a Reply