Ubashiri wangu wiki ya 11 Premier League

Utabiri wangu

WIKI ya 11 ya ligi kuu ya soka nchini England (Premier league) itakuwa ni moja kati ya wiki za nguvu kabisa katika kampeni ya msimu huu wa 2017-18 campaign, kwani timu nne zinazopigiwa upatu wa kushinda taji la msimu zitakuwa zikikutana katika michezo miwili.

Ubashiri wangu wa matokeo ya wiki ya 11 ya premier League.

Jumapili timu kiongozi katika jedwali la msimamo hadi kufikia sasa Manchester City itakuwa mwenyeji wa timu inayojiimarisha ya Arsenal katika dimba la Etihad. Mchezo huo utafuatiwa na ule wa Chelsea kuikaribisha Manchester United, pale Stamford Bridge.

City inaongoza kwa tofauti ya alama katika kilele cha msimamo wa ligi hiyo ikifuatiwa na Manchester United huku Arsenal na Chelsea kila upande ukihitaji matoke kuendeleza matumaini ya nafasi ya kushinda ubingwa wa msimu huu.

Mwenendo chanya wa Arsenal umewafanya mashabiki wa ligi hiyo kuanza kuamini kuwa upinzani katika nafasi nne za juu umeamka upya.

JUMAMOSI NOVEMBA 4

Stoke City vs. Leicester City (1-1)

Huddersfield Town vs. West Bromwich Albion (2-1)

Newcastle United vs. Bournemouth (1-0)

Southampton vs. Burnley (2-1)

Swansea City vs. Brighton & Hove Albion (1-1)

West Ham United vs. Liverpool (0-2)

JUMAPILI NOVEMBA 5

Tottenham Hotspur vs. Crystal Palace (2-0)

Arsenal vs. Manchester City (3-1)

Chelsea vs. Manchester United (1-1)

Everton vs. Watford (1-0)

Be the first to comment

Leave a Reply