Ujio wa Salah, Morata, Abdoulaye Doucoure, Richarlison na wengine kumesaidia kubadilisha utamu wa ladha ya ligi kuu England?

Msimu wa 2016/17 wa ligi ya Premier nchini England jumla ya magoli 1064 yalifungwa, mshambuliaji Harry Kane wa Spurs akishinda mbio za kiatu cha dhahabu kwa kufunga goli 29 na Romelu lukaku aliyekuwa Everton akimfuata nyuma kwa goli 25.

Katika orodha ya msimu huo wengine waliokuwa idadi kubwa ya magoli ni Alex Sanchez 24, Diego Costa 20, Sergio Aguero 20, Dele Alli 18, Zlatan Ibrahimovich 17, Joshua King na Eden Hazard wote goli 16.

Ukiacha Diego Costa anaye elekea Atletico Madrid baada ya sakata lake na meneja wake Antonio Conte kumalizwa na wamiliki wa vilabu vya Chelsea na Atletico huku Zlatan akiendelea kusalia majeruhi, washambuliaji wengine wote wapo.
Hadi kufikia wiki ya saba ya msimu mpya wa ligi kuu ya England tayari jumla ta magoli 173 yameshafungwa na Romelu Lukaku wa Manchester United akiongoza orodha ya wafungaji kwa kupachika wavuni magoli 7.

Je ujio wa washambuliaji wapya ndani ya msimu huu wa 2017/2018 kama vile Alvaro Morata(Chelsea), Mohamed Salah(Liverpool), Abdoulaye Doucoure and Richarlison (Watford) kunaweza kuongeza wingi wa magoli mwisho wa msimu na kuipita idadi ya msimu uliopita?.

Be the first to comment

Leave a Reply