Urusi huru kushiriki Olimpiki

Sasa imebainika ya kuwa Urusi haitofungiwa moja kwa moja kushiriki kwenye michuano ijayo ya Olimpiki baada ya nchi hiyo kuhusika na kashfa ya wanamichezo wake kutumia dawa za kuongeza nguvu wawapo michezoni ambapo Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) imesema sasa suala hilo inaviachia vyama mbalimbali vya michezo ambavyo vinatarajiwa kushirikisha wanamichezo kutoka huko.

Maamuzi haya ya IOC yanakuja kufuatia ripoti iliyotolewa na mhadhiri wa sheria kutoka Canada, Richard McLaren ambaye alisema,”Serikali ya Urusi ilifadhili mpango wa kuwapa wanamichezo wa Urusi dawa za kuongeza nguvu michezoni!”