West Brom dhidi Manchester United ni vita ya Lukaku na Evans

United dhidi West Brom ni vita ya Lukaku na Evans

MSHAMBULIAJI wa Manchester United Romelu Lukaku atakuwa katika wakati mgumu dhidi ya Jonny Evans Jumapili, wakati United itakapo kuwa ikikabiliana na West Brom katika mfululizo wa michezo ya ligi kuu ya Uingereza Jumapili katika dimba la ‘The Hawthorns’.

West Brom itakuwa ikisaka ushindi wa kwanza tangu kuwa chini ya meneja Alan Pardew wakati ikikumbuka ushindi wake wa mwisho katika ligi Agosti 19, tangu hapo haijashinda tena katika michezo 15 iliyofuata.

Kuelekea mchezo huu macho yataelekezwa katika vita ya wawili hao ambao watakuwa wakicheza dhidi ya vikosi vya zamani.

Lukaku atakuwa anarejea West Brom ambako alifunga magoli 17 ya ligi ya Premier wakati huo akiitumikia timu hiyo kwa mkopo akiwa ni mchezaji wa Chelsea msimu wa 2012/13 na atakuwa akikabiliana na Evans ambaye alianza kucheza akiwa United, ambako alishinda mayaji 6 yakiwemo matatu ya ligi ya ligi.

Lukaku alikuwa kwenye ukata wa ufungaji magoli kabla ya kufunga goli la ushindi la United dhidi ya Bournemouth Jumatano katika dimba la Old na kuwa goli lake la 9 katika ligi msimu huu.

Be the first to comment

Leave a Reply