WIKIENDI YA 34 KATIKA PREMIER LEAGUE

BOURNEMOURTH VS MIDDLESBROUGH
BOURNEMOUTH
Bournemouth itakuwa kiaangalia afya ya kiungo wake Dan Gosling ambaye alikosekana katika michezo 3 iliyopita.
Jack Wilshere anaendelea kuwa nje ya msimu kufuatia mpasuko mdogo wa mfupa wa mguu wake hivyo Lewis Cook anaweza kucheza nafasi yake.

MIDDLESBROUGH
Mlinzi Calum Chambers anaweza kupata nafasi baada ya kukosekana kwa wiki 9 kufuatia majeraha ya mguu.
Fabio na Rudy Gestede wako fiti baada ya kusumbuliwa na majeraha madogo lakini Victor Valdes na Grant Leadbitter wataendelea kuwa nje kufuaria maumivu ya mbavu na msuli.

REKODI ZA NYUMA ZA VIKOSI
Bournemouth
Kikosi cha Eddie Howe kinaugulia vichapo 4 mfululizo.
Kimekuwa na wastani wa alama moja katika michezo yao 8 ya mwisho katika uwanja wake wa nyumbani wa Vitality (W2, D2, L4).
Cherries imefungwa magoli 32 tangu kuanza kwa mwaka huu 2017 ambayo ni sawa na kufungwa zaidi ya goli 6 kiazi ambacho ni kikubwa kuliko timu yoyote ya ligi ya Premier msimu huu.
Bournemouth inahitaji alama 8 ili kufikia alama 42 walizoshinda msimu uliopita.

Middlesbrough
Boro imekwenda michezo 15 bila kushinda tangu sikukuu ya Krismas na kushinda alama 6 tu katika kipindi hiki chote ni kiwango cha chini katika daraja la ligi ya Premier.
Ni timu pekee katika ligi 5 kubwa za Ulaya kushindwa kupata ushindi kwa mwaka huu 2017.
Kikosi hicho cha meneja mpya Steve Agnew pia ni kikosi pekee ambacho kimeshindwa kupata ushindi katika kiwanja cha ugenini katika michezo 15, ambapo kimefungwa michezo 7 katika michezo 7 kati ya 9. Kwa mara ya mwisho kupata ushindi ilikuwa katika mchezo dhidi ya Sunderland katika wiki ya pili ya msimu huu.
Kichapo cha bao 4-2 kutoka kwa Hull katika mchezo wao wa mwisho ugenini ulimaliza kiu yao ya kusubiri goli katika uwanja wa ugenini.

SWANSEA VS STOKE CITY
HABARI ZA WACHEZAJI
Nahodha wa Swansea Jack Cork hatakuwepo katika mchezo huu kwa mara ya pili kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya kifundo maulivu yaliyotokana na mchezo dhidi ya West Ham.
Wayne Routledge huenda akahitaji upasuaji wa ‘ hernia’ na Fernando Llorente yuko katika mashaka lakini Leon Britton huenda akapata nafasi ya kucheza kwa mara ya kwanza mwaka huu.
Jon Walters huenda akaanza katika kikosi cha Stoke licha ya kutokufanya mazoezi wiki hii kufuatia matatizo ya mguu.
Joe Allen na Glenn Whelan wanarejea baada ya kusumbuliwa na msuli na mgongo.

Swansea City
Baada ya kupata ushindi katika michezo 5 kati ya 8 ya ligi mfululizo akiwa ameanza kazi Swansea, kocha mkuu Paul Clement sasa amefikisha mchezo wa 6 bila ushindi(D1, L5).
Swansea imeshindwa kufunga katika michezo 4 kati ya 5 ya hivi karibuni.
Ni kikosi ambacho kimefungwa magoli 68 baada ya michezo 33, hakuna timu ilifikisha kiwango hicho cha magoli ya kufungwa katika hatua kama hii halafu ikanusurika kushuka daraja
Gylfi Sigurdsson ametoa pasi za mwisho nyingi za mwisho kutoka na mipira ya kutengwa na kutengeneza nafasi 44 kutokana na mipira ya kutenga.
Stoke City
Stoke ilifanikiwa kuifunga Hull timu hizo zilipokutana kwa mara ya mwisho na kumaliza vipigo mfululizo vya michezo 4.
Aidha Stoke imepoteza michezo 7 katika michezo 9 ya uwanja wa ugenini ikifanikiwa kushinda mchezo mmoja.
Stoke maarufu kama WAFINYANZI haijafunga goli la ugenini tangu Januari 14 pale ilipoifunga Sunderland 3-1.
Inawezekana wakashindwa kufanya hivyo katika mchezo huu ambao utakuwa ni mchezo wa 6 ugenini na itakuwa ni mara yao ya mwanza kushindwa kufanya hivyo tangu April 1985.

Share and Enjoy

Be the first to comment

Leave a Reply