Yanga kucheza na Ihefu raundi ya tatu kombe la FA

Raundi ya tatu ya michezo ya kombe la shirikisho itaikutanisha Yanga na Ihefu

Droo ya raundi ya tatu(3) ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) imechezeshwa leo Januari 5, 2018 ikishirikisha timu 32.

Raundi hiyo ya Tatu imehusisha timu nne(4) za mabingwa wa mikoa timu tatu(3) za Ligi Daraja la Pili,timu Kumi na Mbili (12) za Ligi Daraja la Kwanza na timu 13 za Ligi Kuu.

Mechi za raundi hiyo ya tatu zitachezwa kati ya Jumatano Januari 31, 2018 na Alhamisi Februari 1, 2018

Kabla ya mechi hizo za raundi ya tatu kuchezwa tayari zimechezwa mechi 59 na magoli 137 yamefungwa.

Ratiba

KMC VS TOTO AFRICANS

MAJIMAJI FC VS RUVU SHOOTING

NJOMBE MJI VS RHINO RANGERS

KILUVYA UNITED VS JKT OLJORO

NDANDA VS BIASHARA UNITED

PAMBA SC VS STAND UNITED

POLISI TANZANIA VS FRIENDS RANGERS

JKT TANZANIA VS POLISI DAR ES SALAAM

IHEFU FC VS YOUNG AFRICANS

MWADUI FC VS DODOMA FC

GREEN WARRIORS VS SINGIDA UNITED

TANZANIA PRISONS VS BURKINA

KARIAKOO LINDI VS MBAO FC

MAJIMAJI RANGERS VS MTIBWA SUGAR

KAGERA SUGAR VS BUSERESERE

SHUPAVU VS AZAM FC

Be the first to comment

Leave a Reply