Zanzibar yatinga fainali ya Chalenji kwa kuwafunga watetezi ‘Uganda Cranes’

Allan Kyambadde akikokota mpira wakati kiungo wa Zanzibar akimzonga.

Baraza la vyama vya soka Afrika mashariki na kati CECAFA linasubiri kumtangaza bingwa mpya wa kombe la Chalenji wa mwaka 2017.

Hii inatokana na aliyekuwa bingwa mtetezi na mwenye rekodi ya kuchukua ubingwa huo mara nyingi timu ya taifa ya Uganda (Uganda Cranes) kuondolewa mashindanoni na Zanzibar baada ya kufungwa 2-1 katika mchezo wa nusu fainali ya piliuliochezwa Moi Sports Complex mjini Kisumu leo Ijumaa.

Abdul-Azizi Makame alifunga goli la kuongoza katika dakika ya 22 kufuatia mpira wa kona uliopigwa na Ibrahim Ahmada.

Dakika sita baadaye Uganda Cranes ilisawazisha mshambuliaji aliyechezea timu ya KCCA Derrick Nsibambi.

Uganda Cranes ilisalia na wachezaji 10 uwanjani kufuatia Joseph Nsubuga kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumuangusha mshambuliaji wa timu ya Zanzibar wakati akielekea kumsalimia golikipa wa Cranes akiwa ndani ya eneo la hatari.

Juma Mohammed Issa alifunga goli la penati akiupeleka mpira kushoto na golikipa wa Cranes Watenga akiruka kulia.

Zanzibar itacheza fainali na Kenya Harambee Stars ambayo iliifunga Burundi 1-0 katika dakika za nyongeza katika nusu fainali ya kwanza.

Hiki ndicho kikosi cha timu ya taifa ya Zanzibar kilichotinga fainali ya kombe la Chalenji 2017. Sasa kitaumana na Kenya katika mchezo wa fainali

Zanzibar XI:

Mohamed Abdurahman (G.K), Suleiman Kassim, Ahmed Adeyum, Abdalla Salum, Issa Dau, Abdul Azizi Makame, Mohamed Issa, Yahya Mudathir, Ibrahim Ahmada, Feisal Salum, Ibrahim Said

Subs:

Ahmed Ali (G.K), Nassor Mrisho, Ibrahim Abdalla, Hamad Mshamata, Seif Rashid, Abdalla Haji, Haji Mwinyi

Head Coach: Hemed Suleiman

Be the first to comment

Leave a Reply