Zlatan arejea mazoezini United

Zlatan anarudi baada ya kuwa nje kwa muda mrefu.

Zlatan Ibrahimovic ameungana tena na wachezaji wenzake wa kikosi cha Manchester United wakati akiemdelea kuuguza maumivu yake ya muda mrefu ya mguu.

Mswedishi huyo amekuwa katika majeraha ya mfupa wa maungio ya goti maumivu yaliyotokana na mchezo wa michuano ya Europa dhidi ya Anderlecht mchezo uliofanyika mwezi April Old Trafford.

Imearifiwa na The Sun kwamba Ibrahimovic amekuwa katika mazoezi ya klabuni Carrington akitumia vifaa vya mazoezi pamoja na wenzake kwa wiki sasa na makocha wakionekana kumtambulisha tena kikosini.

Be the first to comment

Leave a Reply